ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 10, 2019

ASASI ZA KIRAIA ZISHIRIKIANE NA SERIKALI MCHAKATO WA BOMBA LA MAFUTA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ameziomba asasi za kiraia kuwa mdau mkubwa kwenye mchakato wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano hasa ujenzi wa bomba la mafuta litokalo  Hoima Uganda hadi Tanga, Tanzania.

Waziri Mhagama alisema hayo kwenye ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu local content katika sekta ya uzinduaji Mikoani  iliyoandaliwa na baraza la uwezeshaji la Taifa na Asasi ya HakiRasilimali inayofanyika Mkoani Shinyanga.

" Tunaziomba asasi za Kiraia zinazofanya kazi katika eneo la mafuta na madini zikiongozwa na HakiRasilimali zitusaidie kwenye kuwaanda watanzania kunufaika na mradi huu wa bomba la mafuta ghafi.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa Bibi Beng'i  Mazana Issa alisema kuwa baraza limeanza tayari kuandaa miundombinu ya kufanikisha mradi huo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bibi Zainabu Telack alisema kuwa, Mkoa wa Shinyanga utanufaika zaidi kwenye warsha hiyo kwa kuwa bomba la mafuta litapita Mkoani humu na kutakuwa na kituo kikubwa cha kuongeza kasi ya msukumo wa mafuta katika Wikaya ya Nzega hivyo wadau wasaidiane kwenye kuwajengea uwezo wananchi ili wachangamkie fursa hizo.

Mwenyekiti wa bodi ya HakiRasilimali Bwana Donald Kasongi alisema kuwa, sera ya local content ndiyo nguzo muhimu ya kunufaika na miradi hii ya kimakati na vyema sasa tuikubali kwa kutunga sheria zake mathubuti.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga bwana Gulam Hafeez Mukadam alisema kuwa kufanyika kwa warsha hiyo Shinyanga ni fursha kwao.

Edwin Soko

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.