ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 10, 2019

WAWEKEZAJI VIWANDA VYA NGOZI WAKARIBISHWA TANZANIA.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Misri ikiwemo kampuni ya Cairo for Investment and Development inayoshughulika na usimamizi wa kiwanda cha ngozi waje kuwekeza nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki kilichoko katika mkoa wa Sharkianchini Misri, ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao waje wawekeze nchini kwani kuna malighafi za kutosha.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi nchini Misri alisema Tanzania ina mifugo mingi hivyo inahitaji wawekezaji watakaojenga viwanda vya kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazo na mifugo hiyo ikiwemo ngozi.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeboresha mazingira ya biashara na ya uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma, hivyo Tanzania ni mahali bora na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kampuni ya Cairo for Investment and Development ya nchini Misri, ambayo inasimamia kiwanda cha ngozi cha Robbiki, Yasser Mohamed Ahmed Al Maghraby alisema kiwanda hicho kinauhitaji mkubwa wa ngozi kutoka Tanzania.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea mradi mkubwa wa mabwawa ya kufugia samaki, mradi wa upanuzi wa awamu ya pili ya mfereji wa suez canal, ambapo aliipongeza Serikali ya Misri kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa kwa kutumia fedha za ndani (Dola bilioni 8.2).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.