ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 12, 2019

MAHAKAMA INAYOTEMBEA KUCHOCHEA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI WA MWANZA.


ILI MAHAKAMA nchini zisiendelee kuonekana kama sehemu ya kupoteza muda wa wananchi ambao badala yake wangeweza kujikita katika shughuli za maendeleo, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imezindua mahakama inayotembea (Mobile Court) ambayo itatoa huduma katika maeneo ya Buswelu, Igoma na Buhongwa ikiwa ni mpango mkakati wa Mahakama Kuu nchini kupunguza changamoto za msongamano wa mashauri mahakamani sanjari na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Akizindua Mahakama hiyo, Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda hiyo ya Mwanza, Sam Rumanyika ambaye alitangulia kwa kutoa Salamu za rambirambi kwa Kampuni ya Azam Media kufuatia msiba wa wafanyakazi wake watano na madereva wawili amesema Mahakama hiyo ni ya kisasa na ya pili nchini na itakayorahisisha utoaji wa huduma na haki kwa wananchi.

Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye alikuwa mmoja wa waalikwa na mdau mkubwa wa Mahakama amesema ili Nchi ifikie malengo yake ya kuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi ni lazima migogoro inayowasilishwa Mahakamani ikamilike kwa haraka na wananchi watumie muda wao mwingi zaidi na rasilimali zao, kuzalisha mali na kutoa huduma badala ya kupoteza muda mwingi wakitafuta utatuzi Mahakamani.Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.