NA ALBERT G.SENGO
Mkutano wa kipekee kati ya rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy umeisha njiani huku ukiacha nyingi sinto fahamu kwa watizamaji waliokuwa wakiufuatilia mubashara baada ya rais huyo wa taifa babe duniani kumtimua kiongozi huyo wa Ukrane. Viongozi hao wawili walihusika katika mazungumzo motomoto na hadharani kuhusu mustakabali wa uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine huku kukiwa na vita vinavyoendelea dhidi ya Urusi. Malumbano hayo makali, ambayo yalijitokeza mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval, yalishuhudia Trump na makamu wa rais wa Marekani J.D. Vance wakimpinga Zelenskyy mara kwa mara, huku kiongozi huyo wa Ukrain akisukuma nyuma hoja zao kwa dharau.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.