ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 28, 2025

KAMPENI YA MSAADA WA SHERIA YA MAMA SAMIA YAWAKOMBOA WANANCHI WA KATA ZA VISIGA NA MISUGUSUGU


 VICTOR MASANGU, KIBAHA

Baadhi ya wananchi katika mitaa mbali mbali iliyopo katika  Kata za Visiga  na misugusugu katika Halmashauri ya Kibaha mji Mkoa wa Pwani wamepatiwa elimu bure juu ya msaada ya kisheria kuhusiana na masuala mbali mbali ikiwemo jinsi ya kutatua migogoro ya ardhi  pamoja na mambo  mengine ya mirathi pamoja na jinsi ya kuweza kupata haki zao za msingi.

Akizungumza na baadhi ya wananchi  wa kata hizo  wakili George Banoba kutoka Wizara ya Katiba na sheria wakati wa mwendelezo wa kampeni ya msaaada wa kisheria ya  Mama Samia amesema kwamba lengo kubwa ni kuwaelimisha wananchi juu ya kuweza kupata haki zao za msingi hasa katika suala zima la maeneo ya ardhi.

Amesema kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto nyingi za wananchi kukosa msaada wa kisheria katika mambo mbali mbali ndio maana Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kuanzisha kampeni hiyo kwa lengo la kuwea kuwasaidia wananchi kupata huduma hiyo ya msaada wa kisheria ambayo  huduma hiyo inatolewa  bure bila malipo.


"Rais wetu wa awamu ya sita  ameweza kuanzisha kampeni hii ya msaada wa kwa katika  amesema kwamba kampeni hiyo imelenga kupita katika maeneo mbali mbali kwa ajili ya kuwaelimisha wwananchi kuweza kutambua haki zao za msingi juu ya suala zima la msaada wa kisheria wa Mama Samia,"alisema Wakili.

Kadhalika  Wakili huyo amewataka wananchi  kuhakikisha wanaepukana kabisa na migogogoro ya ardhi kwa kuzingatia sheria na taratibu zote za nchi ikiwemo kufanya uhakiki wa eneo husika  wanayoyanunua kutoka kwa wataalamu  wa ardhi ambao wataweza kumsaidia kutambua haki zake na kuepukana na migogoro hiyo.


Kadhalika amebainisha kwamba Kampeni ya msaada wa kisheria ya  Mama Samia lengo lake kubwa ni kwa ajili ya kuelimisha wananchi juu ya  masuala ya utatuzi mbali mbali ikiwemo migogogoro ya ardhi, mirathi,ukatili wa kijinsia, kusikiliza kero zinazowakabiliwa wananchi  ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia.

Nao badhi ya wananchi wa Kata ya Visiga akiwemo mzee  Ally Matimbwa kutoka mtaa wa Madafu amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuanzisha kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ambayo itaweza kusaidia kutatua mambo mbali mbali ikiwemo migogoro ya ndoa, pamoja na  migogoro ya ardhi.

Amebainisha kwamba katika baadhi ya maeneo katikaKata ya Visiga tangu mwaka 1984 kuwekuwepo na changamoto kubwa ya migogogro ya ardhi na kwamba kupitia kampeni hiyo ya Mama Samia itaweza kuwa ni mkombozi kutokana na kuweza kupata fursa ya kUupewa elimu juu ya masuala ya kisheria.
Diwani wa kata ya Visiga Kambi Legeza (kulia aliyenyoosha mkono juu) amesema kwamba uwepo wa kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imekuja wakati muafaka kwani  itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi ambao walikuwa wanakaboliwa na changamoto katika masuala ya kisheria na ukosefu wa kupata haki zao za msingi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.