ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 24, 2025

WAZIRI MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA UJENZI SGR MWANZA - ISAKA

 NA ALBERT G.SENGO/MALAMPAKA/SIMIYU

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amelitaka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kutumia uzoefu wa uendeshaji wa reli ya SGR Dar Es Salaam - Dodoma katika kufanya maboresho kwenye ujenzi wa reli ya SGR kipande cha tano (Lot 5) Isaka - Mwanza ili kuepuka usumbufu usio wa lazima. Prof. Mbarawa ameyasema hayo leo alipotembelea mradi huo kwa lengo la kujionea maendeleo na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mradi huo wa kisasa unaotarajiwa kuleta mapinduzi katika nyanja ya usafiri na usafirishaji nchini. " Tunataka yale tuliyojifunza kule hapa yasijirudie tena, kwa mfano Dar es Salaam kuna changamoto ya maegesho ya magari pamoja na Dodoma sasa kwenye mikoa hii tuhakikishe tunajipanga vizuri hata watu wakiongezeka kusiwe na shida," Amesema Mbarawa. Aidha Waziri Mbarawa amesema kwa upande wa serikali watahakikisha wanamsimamia vizuri mkandarasi pamoja na kumpatia malipo kwa wakati ili mradi huo ukamilike kwa wakati na wananchi wanufaike kama Dar es salaam, Morogoro na Dodoma wanavyonufaika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.