IMEANDIKWA NA VICTOR MASANGU, PWANI KUSOMWA NA ALBERT G.SENGO Mashirika mbali mbali ya umma nchini yameaswa kuwa na uzalendo kwa kuepuka tabia ya kuwa tegemezi wa fedha za ruzuku kutoka serikalini na badala yake Mashirika hayo yajenge mikakati imara ya kuweza kuleta mageuzi katika kuichangia gawio serikali katika mfuko wa hazina kwa ajili ya kuleta chachu ya maendeleo na kuongeza Pato la Taifa. Kauli hiyo imetolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichele, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha siku mbili kilichowakutanisha 0fisi ya msajiili wa hazina, Ofisi ya Taifa ya ukaguzi na baadhi ya viongozi wa mashirika ya umma. Aidha Mkaguzi huyo ameongeza kuwa kikao kazi hicho kimelenga kuwajengea uwezo watumishi wa mashirika ya umma pamoja na kuweka mikakati kabambe ya kuimarisha mifumo ya utekelezaji wa majukumu ya uongozi ikiwa sambamba na kuzilinda rasilimali za Taifa kwa maslahi ya wananchi sambamba na kuepuka kabisa mianya ya upotevu wa mapato ya serikali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.