Amavubi ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 17 kupitia kwa Domicique Nshuti dakika ya 18 kabla ya Himid Mao kuisawazishia Taifa Stars dakika ya 34 kwa mkwaju wa penalti.
Matokeo hayo yanaipa wakati mgumu Taifa Stars, kwani inatakiwa kushinda katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumamosi ijayo jijini Kigali Rwanda.
Taifa Stars ikifanikia kushinda katika mchezo huo wa marudiano itasonga mbele katika hatua nyingine ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) zitakazofanyika Kenya mwakani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.