ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 30, 2016

JIMBO LA CHATO LACHANGIWA NA WADAU WA MAENDELEO JIJINI MWANZA SH MILIONI 305.7 ZA KUTENGENEZEA MADAWATI



















NA:- PETER FABIAN MWANZA
MBUNGE wa Jimbo la Chato, Dk Medard Karemani achangisha na kufanikiwa kukusanya kiasi cha Sh milioni 305.7 kwa ajili ya kusaidia utegenezaji wa upungufu wa madawati 10,000 yanayotakiwa katika shule za msingi 131na sekondari 28 jimboni humo.
Dk Karamani alisema kwamba hali ya wanafunzi kukaa chini katika jimbo la Chato linatokana na tamko la serikali la Elimu kutolewa bure na kusababisha wanafunzi walioandikishwa kuingia shuleni kuongezeka kwa aslimia 150 jambo ambalo limeleta mahitaji ya madawati 28,000 .
“Tulihamasisha wananchi na wadau wengine kuchangia na kufanikisha kutengeneza madawati 18,000 hivyo tunahitaji kutengeneza madawati 10,000 ili kukabiliana na changamoto hiyo wanafunzi 100,000 wanaosoma kuweza kukaa kwenye madawati wakati wa kusoma madarasani,”Alisema.
Mgeni rasmi katika harambee hiyo iliyofanyika juzi jijini Mwanza, Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Wasanii, Nape Moses Nnauye, alisema kwamba ni wajibu wa Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Wilaya kushirikiana kuhamasisha wananchi kujitokeza kuiunga mkono kuchangia maendeleo.
“Rais Dk John Magufuli alisitisha michango yenye kero kwa wananchi lakini wananchi wanaweza kushiriki kuchangia kwa hiali miradi ya maendeleo iliyopo katika maeneo yao kwa kushirikiana na serikali, hivyo viongozi na wawakirishi wa wananchi tunao wajibu wa kuwahamasisha ili kutekeleza kwa ufanisi miradi na kupata huduma zinazositahili,”alisema.
Nnauye alisema kwamba suala la madawati linahitaji kuwepo msukumo wa kuwaelimisha wananchi kuchangia madawati pamoja na kuwashirikisha wadau mbalimbali ndani ya wilaya, mkoa na nje ya mikoa ili kufikia malengo yanayotokana na changamoto hiyo ambapo binafsi naunga mkono kwa mchango wa Sh milioni nne huku baadhi ya marafiki wakiwa nao wanachangia .
Katika harambe hiyo Kampuni ya Busolwa mine ya Mkoani  Geita ilichangia madawati 1,000, Saimon Group madwati 1,000,  Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM taifa (NEC) Christopher Gachuma madawati 300,  Dk Karamani Sh milioni 4, Kampuni ya Waja dawati 500, baadhi ya Wabunge wa Kanda ya Ziwa walioalikwa kila mmoja milioni moja huku baadhi ya Kampuni za wachimbaji wadogo wa madini wakichangi.

Waziri Nnauye akitangaza matokeo ya michango ya fedha zilizopatikana katika harambe hiyo ya kuchangia madawati katika jimbo la Chato yaliyoratibiwa na Dk Karemani alisema kwamba waalikwa wakiwemo wadau na wa Wilaya ya Chato na kutoka maeneo mbalimbali nchini kuunga mkono na kupatika fedha taslimu Sh milioni 120.

Alieleza wachangiaji kuwa zingine ni ahadi na jumla kuu ya michango yote kufikia kiasi cha Sh 305,721,500/=. Ambazo zitaendelea kutekeleza ukamilishwaji wa madawati katika Jimbo lote la Chato na kutoa wito wadau kuendelea kuhamasika kuchangia pindi wakifuatwa tena na kukamilisha ahadi zao kwa kipindi kifupi ili kukamilisha zoezi hilo ifikapo Agusti 30 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.