KIFO CHA NGULI WA MUZIKI WA POP DUNIANI KIMEZUA MASWALI MENGI KUHUSU NINI KILISABABISHA AFYA YAKE KUBADILIKA HATIMAYE KIFO, NA HATA NINI HATMA YA JAMII ILOKUWA IKIMTEGEMEA. WATOTO WAKE WATATU ALOWAACHA NI MIONGONI MWA WATU WANAOTAJWA ZAIDI. NAMNA GANI WATAISHI, NANANI ATAKAYEKUWA MLEZI BAADA YA BABA YAO KUAGA DUNIA? DEBBIE ROWE NESI ALIYEOLEWA NA MICHAEL 1996 NAKUTALIKIWA 1999 NA MAMA WA PRINCE MICHAEL(12) NA PARIA(11) NA PRINCE MICHAEL II (aka BLANKET) HUYU ANARIPOTIWA KUWA ALIZALIWA NA MAMA AMBAYE MPAKA LEO JINA LAKE HALIJATAMKWA HADHARANI. MSEMAJI MKUU WA JACKSON AMBAYE PIA NI RAFIKI WA FAMILIA BWANA BRIAN OXMAN AMEMTAJA MAMA MZAZI WA MICHAEL (pichani kulia) NDIYE ATAKAYEKUWA MWANGALIZI WA WATOTO KWA SABABU ANAWAJUA KIUKARIBU NA AMEKUWA AKIKAANAO MARA KWA MARA. YOTE HAYA YANASEMWA LAKINI KWA VYOVYOTE VILE KUNA JAMBO LITAZUKA TOKA KWA DEBBIE ROWE MAMA WA WATOTO.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.