ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 28, 2017

WATAALAMU WATANGAZA DAWA YA KUKINGA UKIMWI, MKUTANO WA KIMATAIFA WA UKIMWI, PARIS

Wataalamu walioshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Ukimwi uliofanyika Paris nchini Ufaransa wametangaza mbinu mpya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV na kutibu maradhi ya Ukimwi.

Ripoti zinasema mkutano huo ambao ulimaliza kazi zake usiku wa kuamkia leo, ulihitimishwa kwa kutangazwa habari za mafanikio ya kuzuia na kutibu maradhi ya Ukimwi.

Washiriki katika mkutano huo wanasema dawa hiyo mpya ya Ukimwi imetengenezwa kwa namna ambayo inapambana na virusi vya HIV na kuvifubaza, na kwamba mafanikio haya ni habari nzuri kwa watu wenye virusi hivyo au wale wenye ndugu na jaa walioathirika.
Ukimwi umeua zaidi ya watu milioni 35 duniani

Chris Beyrer wa jumuiya ya The International AIDS Association anasema kuwa, mtu mwenye mume au mke aliyeathiriwa na virusi vya Ukimwi anaweza kutumia vidonge vyake vya kila siku au kudunga sindano mara moja kwa miezi mwili na hivyo kuzuia kabisa uwezekano wa kupatwa na virusi hivyo. Amesisitiza kuwa, hayo ni mafanikio na mapinduzi makubwa katika vita na mapambano dhidi ya Ukimwi.

Nchi ya Swaziland barani Afrika ndiyo inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waathirika wa virusi vya Ukimwi na unaripotiwa kuwa, mtu mmoja kati ya kila watu watatu ameambukizwa virusi hivyo

Zaidi ya watu milioni 35 wamepotea maisha tangu vurusi vya HIV na Ukimwi ulipoeneza duniani katika miaka ya 1980.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.