Polisi ya Pakistan imeamuru kutiwa nguvuni
wajumbe 20 wa Baraza la kijiji kimoja cha katikati mwa nchi hiyo baada
ya wajumbe hao kutoa hukumu ya kubakwa na kunajisiwa binti mwenye umri
wa miaka 17 ili kulipiza kisasi cha uhalifu kama huo uliofanywa na kaka
yake.
Suala
hilo limefichua zaidi hali inayotawala mfumo wa kikabila nchini
Pakistan. Kamanda wa Polisi ya eneo hilo, Saliim Khan Niyazi amesema
kuwa, msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 alibakwa na kunajisiwa
katika mji wa Multan katika jimbo la Punjab.
Baraza
la kijiji hicho liliamuru msichana huyo abakwe ili kulipiza kisasi cha
kitendo kilichofanywa na kaka yake cha kumbaka msichana mwingine katika
eneo hilo. Msichana huyo alikamatwa na kubakwa mbele ya wazazi wake.
Mabaraza ya vijiji yanatambuliwa kuwa ni mbadala wa mahakama dhaifu za Pakistan ambazo huchelewesha kesi zinazowasilishwa huko kwa miaka mingi. Maamuzi ya mabaraza hayo yanayotegemea ada za kikabila, yanakubaliwa na wakazi wa maeneo ya vijijini, ingawa hayatambuliwi rasmi na serikali ya Pakistan.

Kamada
wa Polisi, Saliim Khan Niyazi amesema mkuu wa baraza hilo lililotoa
hukumu ya kubakwa msichana huyo na wajumbe wengine 20 wametiwa nguvuni
na kwamba mtuhumu mkuu ametoroka.
Mkuu wa jimbo la Punjab, Shahbaz Sharif ameliamuru jeshi la polisi kuwasaka na kuwakamata wajumbe wote wa baraza la kijiji hicho
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.