MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga U20,Yusuph Nyamiundu, (katikati),
akijaribu kuwatoka mabeki wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Hisani wa
kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20
walishinda mabao 3-0. Picha na Muhidin Sufiani
MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga U20,Paul Godfrey, (kulia), akimtoka
mchezaji wa Mbeya City, Anthony, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia
Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao
3-0. Picha na Muhidin Sufiani
BEKI wa timu ya Yanga U20, Mawazo Gawasa, (kushoto) akiwadhibiti
wachezaji wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko
wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0.
Picha na Muhidin Sufiani
BEKI wa timu ya
Yanga U20, Mawazo Gawasa, (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji
wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini
wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai
27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0. Picha na
Muhidin Sufiani
BEKI wa timu ya Yanga U20,
Bakari Jomba, (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Mbeya
City 'Demba Ba', wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa
Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0.
Kulia ni Saad Awadh, akijiandaa kutoa msaada. Picha na Muhidin Sufiani
BEKI wa timu ya Yanga U20, Mawazo Gawasa, (kushoto) akimdhibiti winga
wa Mbeya City, Idd Nabe, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko
wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0.
Picha na Muhidin Sufiani
YANGA U20 YAWADUWAZA MBEYA CITY FC WAKIWA KAMILI UWANJA WA SOKOINE MBEYA NA KUTANGULIA FAINALI
NA MUHIDIN SUFIANI, MBEYA
TIMU
ya Vijana ya Yanga U20 jana iliwashangaza mashabiki wa soko
waliojitokeza kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kuacha gumzo
baada ya kuwaduwaza Mbeya City wanaoshiriki Ligi Kuu Bara kwa kuwachapa
mabao 3-0 katika mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa
UKIMWI.
Mechi
hizo za Hisani zimeandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi
Tanzania TACAIDS, ambapo zinashirikisha jumla ya timu Nne za Yanga U20
na Simba U20 kutoka jijini Dar es Salaam, huku Mbeya City na Tanzania
Prisons zikiwa ni zile zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.
Kabla
ya mchezo huo kuanza wakati timu zikipasha misuli, mashabiki
waliokuwapo uwanjani hapo baadhi walisikika wakijutia kuingia uwanjani
kwa kuhisi kukosa burudani, lakini kadri mchezo ulivyokuwa ukiendelea
baadhi ya mashabiki walianza kubadilika na kuanza kuwashangilia vijana
hao wa Yanga U20, waliokuwa wakionyesha kandanda safi na kuwainua vitini
mashabiki wa Soka wa jiji la Mbeya.
Katika
mchezo huo uliokuwa wa kuvutia tayari Yanga wametangulia fainali na
kusubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Simba U20 na Tanzania Prisons
ambapo fainali hiyo itachezwa siku ya Jumamosikwenye Uwanja wa Sokoine.
Mabao
ya Yanga yalifungwa na Maka Edward, katika dakika ya 30 kipindi cha
kwanza, akimalizia pasi nzuri ya Said Mussa na dakika ya 64 kipindi cha
pili kwa mkwaju wa penati, baada ya kipa wa Mbeya City, Fikirini Bakari,
kumchezea rafu mshambuliaji wa Yanga,Paul Godfrey, ndani ya eneo la
hatari, huku pazia la mabao likifungwa na Festo Greyson, katika dakika
ya 79 baada ya kazi nzuri ya Paul Godfrey, aliyemtoka beki wa kushoto wa
Mbeya city na kupiga krosi nzuri iliyozaa bao hilo.
Akizungumzia
matokeo hayo Kocha msaidizi wa Mbeya City Mohamed Kijuso, alisema kuwa
kwa upande wake amechukulia ni matokeo ya kawaida na kutokana na kwamba
hakuna wanachopoteza bali ilikuwa ni kipimo tosha kwa wachezaji wake
ambao baadhi ni wageni waliojiunga na timu msimu huu kujiandaa na msimu
mpya wa Ligi Kuu na kuongeza kuwa ameona mapungufu mengi ambayo
atayafanyia kazi na Kocha mkuu atakayejiunga na kikosi hicho.
''Kikubwa
ni mazoezi kwani tayari nimeona mapungufu ndani ya kikosi changu,
nitayafanyia kazi na Kocha atakayejiunga nasi hapo baadaye, ila
mashabiki watambue kuwa haya ni matokeo tu ya mchezo na hakuna
atulichopoteza kwani ulikuwa ni mchezo wetu wa kwanza kujiandaa na
kuangalia kikosi chetu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu''. alisema
Kijuso.
Kwa
upande wake Kocha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema kuwa
amefurahishwa na matokeo hayo ambayo alikuwa akiyatarajia baada ya kuona
wapinzani wake wamepanga Kikosi cha Ligi Kuu, huku yeye akiwaamini na
kuwapa majukumu Vijana wa U20, ambao hawakumuangusha baada ya kufuata
maelekezo waliopewa.
''Kwa
kweli Vijana wangu wamenifurahisha sana na matokeo haya kwa upande
wangu kama mwalimu niliyatarajia na hasa baada ya kuona wapinzani wakiwa
na kikosi cha wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu, kwani nilijua watacheza
kwa kuwazania vijana wangu na kujiamini sana jambo ambalo vijana wangu
walilitumia kuwashangaza na hawakuamini kilichowakuta katika dakika 90
za mchezo,
Mimi
nilikuwa na vijana wawili tu walicheza ligi msimu uliopita na mmoja
ambaye amepandishwa msimu huu, lakini niliwaamini zaidi vijana na
kuwapangia Mhilu tu aliyeshiriki ligi iliyopita ili kuwapa hamasa
wenzake jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa'', alisema Nsajigwa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.