Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI
Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda (katikati) akimkabidhi Jezi Meneja
wa Vifaa wa timu ya Yanga, Mohamed Mposo, wakati wa zoezi la kukabidhi
vifaa vya michezo kwa ajili ya kushiriki Mechi za Hisani kwa ajili ya
kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI. Makabidhiano hayo yamefanyika leo
asubuhi ndani ya Ofisi za Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo mchezo
wa kwanza utakuwa ni kati ya Yanga na Mbeya City utakaochezwa leo
jioni, na mchezo wa pili utakuwa ni Simba na Tanzania Prisons
utakaochezwa kesho na fainali itachezwa siku ya Jumamosi kwa
kuzikutanisha timu washindi wa mchezo wa leo na wa kesho. Kushoto ni
Mratibu wa Mechini hizo, Emmanuel Petro na Teddy Mapunda (kulia) ni
Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya. Picha zote na Muhidin Sufiani
Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI
Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda (katikati) akimkabidhi Jezi Meneja
wa timu ya Mbeya City, Geofrey Katepa, wakati wa zaoezi la kukabidhi
vifaa vya michezo kwa ajili ya kushiriki Mechi za Hisani kwa ajili ya
kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI. Makabidhiano hayo yamefanyika leo
asubuhi ndani ya Ofisi za Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo mchezo
wa kwanza utakuwa ni kati ya Yanga na Mbeya City utakaochezwa leo
jioni, na mchezo wa pili utakuwa ni Simba na Tanzania Prisons
utakaochezwa kesho na fainali itachezwa siku ya Jumamosi kwa
kuzikutanisha timu washindi wa mchezo wa leo na wa kesho. Kushoto ni
Mratibu wa Mechini hizo, Emmanuel Petro na Teddy Mapunda (kulia) ni
Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya.Tz Prisons:- Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa
Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda
(katikati) akimkabidhi Jezi Meneja timu ya Tanzania Prisons, Havinitishi
Abdallah (wa pili kulia) wakati wa zaoezi la kukabidhi vifaa vya
michezo kwa ajili ya kushiriki Mechi za Hisani kwa ajili ya kuchangia
Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI.
Makabidhiano hayo
yamefanyika leo asubuhi ndani ya Ofisi za Uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya, ambapo mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya Yanga na Mbeya City
utakaochezwa leo jioni, na mchezo wa pili utakuwa ni Simba na Tanzania
Prisons utakaochezwa kesho na fainali itachezwa siku ya Jumamosi kwa
kuzikutanisha timu washindi wa mchezo wa leo na wa kesho. Kushoto ni
Mratibu wa Mechini hizo, Emmanuel Petro na Teddy Mapunda (kulia) ni
Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI
Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi
Meneja timu ya Simba SC, Nico Nyagawa (wa pili kulia) wakati wa zaoezi
la kukabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya kushiriki Mechi za Hisani
kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI. Makabidhiano hayo
yamefanyika leo asubuhi ndani ya Ofisi za Uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya, ambapo mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya Yanga na Mbeya City
utakaochezwa leo jioni, na mchezo wa pili utakuwa ni Simba na Tanzania
Prisons utakaochezwa kesho na fainali itachezwa siku ya Jumamosi kwa
kuzikutanisha timu washindi wa mchezo wa leo na wa kesho. Kushoto ni
Mratibu wa Mechini hizo, Teddy Mapunda (kulia) ni Katibu wa TFF Mkoa wa
Mbeya.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
TIMU
za Yanga na Simba, U20 zimewasili jijini Mbeya kwa ajili ya kushiriki
mechi za Hisani maalumu kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI,
zinazoanza kutimua vumbi jioni ya leo kwenye Uwanja wa Sokoine jijini
hapa.
Akizungumzia
maandalizi ya mechi hizo Msemaji wa TACAIDS na Mkuu wa Kitengo cha
Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Elizabeth
Kaganda, alimesema kuwa timu za Yanga na Simba kutoka jijini Dar es
Salaam, tayari zimewasili jijini hapa, na zipo katika hali nzuri kwa
mechi hizo.
''Tunashukuru
mungu timu zote zimefika salama kwa ajili ya kushiriki mechi hizo za
Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, na tunatarajia kupata
burudani safi ya soka kutoka kwa timu zote kutokana na maandalizi
waliyofanya, ambapo mshindi atakabidhiwa kikombe, ambapo timu zote
zimejitolea kushiriki bila malipo''. amesema Kaganda
Aidha
alisema mchezo wa kwanza utaanza leo kwa kuzikutanisha timu za Yanga na
Mbeya City, na kesho itakuwa ni Simba na Tanzania Prisons, fainali
itachezwa siku ya Jumamosi ambapo mshindi wa mchezo wa leo atacheza na
mshindi wa mchezo wa kesho, na mechi zote zikipigwa katika Uwanja wa
Sokoine majira ya saa tisa na nusu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.