William Ruto Apata Pigo Jingine Huku Mahakama Ikipiga Breki KDF Kutumiwa Kuzima Maandamano ya Gen Zs
Rais William Ruto amekumbwa na msukosuko mkubwa katika mpango wake wa kupeleka wanajeshi wa Kenya badala ya polisi kuzuia ghasia katika maeneo mbalimbali nchini.
Mnamo Jumatano, Juni 26, Chama cha Wanasheria nchini (LSK) kilishtaki Waziri wa Ulinzi Aden Duale na Bunge la Kitaifa kuhusu kutumwa kwa KDF kufuatia maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha. LSK iliiomba mahakama kusitisha uamuzi huo kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi hiyo.
Mahakama iliamuru pande zote kufika kwa ajili ya kusikilizwa kwa muda mfupi ombi hilo, ambalo liligombanisha LSK dhidi ya Serikali na Waziri wa Ulinzi.
Katika stakabadhi zilizowasilishwa kortini, LSK inasema kwamba Rais William Ruto hajatangaza hali ya hatari chini ya Kifungu cha 58 cha Katiba katika kutekeleza mamlaka yake ya kikatiba chini ya Kifungu 132 (4) (d) cha Katiba.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.