NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon amempongeza Rais kwa kuweza kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 4 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa daraja jipya la kudumu katika mto mpiji ambalo litaweza kuwa mkombozi kwa wananchi kuvuka bila shida hasa katika kipindi cha mvua.
Darala hilo la mto mpiji ambalo kwa sasa limejengwa kwa muda limekuwa ni kiunganishi na mkombozi mkubwa kwa wananchi kutoka Wilaya mbili za Kibaha Mkoa wa Pwani pamoja na Wiyaya ya Ubungo ya Jijini Dar es Salaam
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa pongezi hizo wakati wa halfa fupi ya kukabidhiwa daraja la muda kutoka kwa kaimu mkuu wa mafunzo na operesheni wa Jeshi la la nchi kavu Brigadia Jenerali Stanley Mjelwa halfa ambayo imehudhuliwa na viongozi wa serikali,chama,wananchi na Tarura.
Nikson amebainisha kwamba pia amemshukuru kwa dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka kwa kuwa mstari wa mbele katika kulipambania kwa hali na mali ujenzi wa daraja hilo liweze kujengwa ili wananchi waweze kupita kwa urahisi.
Amesema kwamba Mbunge Koka amepambana na kuwasemea wananchi wa Pangani juu ya adha wanayoipata ndio maana Rais Samia ameweza kuwa msikivu na kukubali kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa ujenzi wa daraja hilo la kudumu.
Mkuu huyo amefafanua kwamba kwa sasa daraja ambalo limejengwa na Jeshi la nchi kavu litatumika kwa muda na baada ya hapo litajengwa daraja lingine jipya la mto mpji kwa fedha ambazo zimetolewa na Rais Samia kiasi cha shilingi bilioni 4
"Kwa kweli nimshukuru sana Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutupatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja la kudumu katika mto mpiji licha ya kutoa fedha zingine zaidi ya milioni 250 kwa ajili ya kukarabati daraja la muda nimshukuru sana"
"Pia Mbunge wetu wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuwa mstari wa mbele katika kuomba fedha na kuchangia michango mbali mbali katika daraja la muda ambalo limekabidhi kwangu leo hii ni juhudi za Mbunge Koka ili wananchi waweze kupata daraja hilo,"alisema Nickson.
Pia amesema kwamba anawashukuru Tarura pamoja kwa juhudi zao pamoja na Jeshi la nchi kavu kwa kuweza kukamilisha ujenzi huo wa daraja la muda katika mto mpiji.
Naye Kaimu wa mkuu wa mafunzo na operesheni wa Jeshi la nchi kavu Brigedia Jenerali Stanley Mjelwa ameitaka Tarura kuhakikisha wanalifanyia ukarabati daraja hilo ili liweze kuharibika mapema.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) Wilaya ya Kibaha mjini Injinia Samwel Ndoveni amesema kwamba daraja hilo la awali limeweza kufanyiwa marekebisho ili kuweza kuwapa fursa wananchi wa Wilaya ya Kibaha na Wilaya ya Ubungo waweze kupita kwa urahisi zaidi.
Nao baadhi ya wananchi wa kata ya pangani hakusita kuzungumzia jinsi ya Mbunge wa Jimbo lao alivyoweza kuwa na wananchi bega kwa bega katika ujenzi wa daraja hilo la mto mpiji.
Wamesema kwamba Mbunge Koka tangu mwanzoni ameshirikiana na diwani wa kata ya Pangani pamoja na wananchi kwa ajili ya kuweza kuhakikisha daraja hilo la muda linakamili na kupitika kwa urahisi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.