NA ALBERT G.SENGO
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amemshauri mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kusikiliza ushauri wa familia yake wa kumtaka kutogombea tena nafasi hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema hii leo Jumanne, Januari 14, 2025 Lema amesema anamheshimu Mbowe kutokana na kazi kubwa ya kukijenga chama hicho, lakini kwa sasa asikilize zaidi ushauri wa familia yake. Lema amesema Mbowe mara kadhaa amekuwa na nia ya kupumzika na kuwaachia nguvu mpya vijana kuendeleza mapambano, lakini watu wanaoitwa wanachama wamekuwa wakimshauri kuendelea kuwa mwenyekiti.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.