ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 16, 2025

RAIS SAMIA AFANYA KWELI KIBAHA TC ATOA PIKIPIKI 37 KWA MAAFISA UGANI

 
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

 
Halmashauri ya Kibaha mji imepokea jumla ya pikipiki zipatazo  37 kutoka serikalini kupitia Wizara ya kilimo kwa lengo la  kuwawezesha maafisa ugani wa kilimo kutoka kata zote 14 kwa ajili ya  kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi na  ufanisi zaidi katika suala la kuwahudumia wakulima na kuleta matokeo chanya katika sekta ya kilimo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha  Nickson John  wakati wa halfa ya kukabidhi pikipiki hizo 37 kwa maafisa ugani hao na kuwatka kuhahakikisha kwamba wanaweka misingi ya kuwa na mikakati kabambe katika kuwa  na  kilimo cha kisasana chenye kuleta tija kwa wakulima.
Mkuu huyo alisema kwamba lengo kubwa la serikali ni kuhakikisha wanaendekea na kufanya juhudi za hali na mali za kuhakikisha inaendelea kuwasajili wakulima wote waweze katika mfumo ambao unatambulika ikiwemo sambamba na kuwapatia pembejeo za kilimo ambazo zitaweza kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Tunapenda kumshukuru kwa dhati Rais wetu wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo pamoja na kutoa vitendea kazi hivi amabvyo ni boda boda 37 kwa maafisa ugani kwa lengo la kuweza kuongeza ufanisi na tija  zaidi katika suala zima la kuwahudumia wakulima waweze kuwa na kilimochenye tija katika maeneo yao,"alisema Simon.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha kwamba nia kubwa ya serikali ni kushiikiana bega kwa bega na maafisa ugani katika kuweka mippango endelevu ya kufanya kilimo cha kisasa ambacho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakulima pamoja na wananchi kwa ujumla katika sekta ya kilimo.

Katika hatua nyingine amewaagiza maafisa ugani pamoja na wataalamu wakilimokuhakikisha kwamba wanazitumia vizuri pikipiki hizo kwa kuwafikia walengwa ambao ni wakulima na kwamba dhima kubwa ya serikali ni kuona  kunatokea mabadiliko  zaidi katika maeneo mbali mbali ya Kibaha mji.
 
Pia Mkuu huyo amemshukuru kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezeha vyombo hivyo vya usafiri ambavyo vitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutimiza majukumu ya maafisi ugavi hao  ikiwemo pamoja na kuongeza kiwango cha mapato.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kibaha mji Dkt. Rogers Shemwelekwa amebainisha kwamba kwa sasa kuna jumla ya watumishi wa ugani wa kilimo wapatao 41 ambao wanatoa ushauri wa ugani kwa wakulima 7, 528 katika mitaa yote  73 kutoka kata 14.
Pia mkurugezni huyo amebainisha kwamba  kwa sasa halmashauri ya mji Kibaha lina eneo linalofaa kwa kilimo lenye ukumbwa wa wastani wa Hekta zipatazo 7, 750 na kwamba wakulima 3,600 tayari wameorodheshwa katika mfumo wa mbolea na mbegu  za ruzuku katika msimu kwa mwaka 2024/2025 na wanapata mbolea na mbegu za ruzuku.

Pia amesema kuwa Halmashauri ya mji Kibaha kuna fusa mbali mbali na kwamba kuna wakulima wapatao  191 wa zao la korosho  wamefaanikiwa kupata  ruzuku kwa ajili ya zao hilo, ambapo pia wakulima wapatao 6, 709 ni wale wa mbogamboga , na wakulima 628 ni wa mazao ya matunda.
Nao baadhi ya maafisa Ugani katika Halmashauri ya Kibaha mji wamempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwawezesha vitendea kazi hivyo vya pikipiki zipatazo 37 ambazo zitaweza kuwasaidia katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yao ya kuwahudumia wakulima katika maeneo yao.

Wamebainisha kwamba hapo awali walikuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya usafiri na kupelekea kushindwa kufika kwa urahisi kwa wakulima lakini kwa sasa wataweza kufanya kazi zao kwa uafanisi mkubwa na kuwafikia  wakulima wao kwa urahisi na kutekeleza maelekezo ya serikali ya kuwahudumia wakulima na kuwa na kilimo chenye tija.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.