Mafundi wakiwa kazini kuendelea na ukarabati wa majengo ya shule hiyo ya msingi Mapinduzi English medium iliyopo manispaa ya Iringa.
Mwenyekiti wa shule ya msingi Mapinduzi
English medium Haliel Abdallah akiwa na kiongozi mwingine kwenye kama hiyo wakikagua ukarabati ambao unaendelea
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wazazi wa shule ya msingi Mapinduzi
English medium iliyopo manispaa ya Iringa wameamua kuikarabati ili kuboresha
mazingira ya shule kwa lengo la kukuza taaluma ya wanafunzi katika shule hiyo.
Akizungumza na blog hii
mwenyekiti wa shule hiyo,Haliel Abdallah alisema kuwa shule hiyo ilikuwa na miundombinu
mibovu ambayo ilikuwa sio rafiki kwa walimu na wanafunzi hivyo ilikuwa
inachangia kutoingia kwenye shule nyingine za aina hiyo.
“Kwa kifupi sana kamati
ilibaini kwamba mazingira ya madarasa pamoja na ofisi za walimu hazikuwa rafiki
hivyo tukaamua kuanza kufanya tathimini kwa lengo la kuanza kukarabati shule
hiyo ili irudi kwenye ubora kama uliokuwepo hapo awali” alisema Abdallah
Abdallah alisema kuwa lengo la
kujenga darasa jipya katika shule hiyo ili kupanua wigo wa kuwa na vyumba vingi
ambavyo vitatuasaidia kuleta ushindani na shule nyingine zenye mchepuo wa
masomo ambayo yanafundishwa kwa lugha ya kingereza
“Tunataka kuhakikisha kuwa
shule hii inakuwa kwenye ubora wa hali ya juu kwenye miondombinu kuanzia madarasa,ofisi
za walimu na mazingira ya shule lazima yawe ya kuvutiwa kwa walimu,wanafunzi na
hata wazazi wawe wanajisifia watoto wao kusoma katika shule hiyo” alisema Abdallah
Abdallah aliongeza kwa kusema
kuwa katika ukarabati huo utahusisha pia ukarabati wa madawati pamoja
kuhakikisha walimu wanakuwa na samani
bora ambazo nazo zinakuwa rafiki na mazingira ya kufundishia na
kuandalia masomo.
Aidha Abdallah amewapongeza
wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule hiyo kwa kujitoa kukakikisha
shule hiyo inakarabatiwa kwa lengo la kuwa nashule yenye kushindana na shule
nyingine zilizopo mkoani Iringa na nje ya Iringa.
Awali akitoa taarifa ya hali
ilivyokuwa hapo awali walimu mkuu wa shule hiyo Emanuel Mwakyusa alisema kuwa
miundombinu ya shule hiyo haikuwa rafiki kwa kutoa elimu iliyobora kwa kuwa
madarasa na majengo mengi yalikuwa chakavu sana.
“Madarasa mengi yakuwa chakavu
hivyo ikawa ngumu kufanya usafi kukiwa na mashimo,paa zilikuwa zimechoka na
kuvujisha maji kipindi cha vua hiyo hali ya usafi ilikuwa mbaya na kusababisha
kutoa elimu ambayo ilikuwa haistahili” alisema Mwakyusa
Mwakyusaalisema kuwa ukarabati
huo umefanywa na wazazi tu bila kuigusa serikali kwa kuwa wazazi hao wanapenda
kufanya maendeleo kwa lengo la kuhakikisha waoto wao wanasoma katika mazingira
yaliyo bora.
“Mimi niwapongeze wazazi ambao
watoto wao wanasoma katika shule hii kwa kujitoa kwa moyo wao wote kuhakikisha
kuwa shule hii inakarabatiwa vilivyo na kuwa na mazingira yaliyo bora” alisema Mwakyusa
Mwakyusa alisema kuwa ukarabati
huo utasaidia kukuza taaluma za wanafunzi wa shule hiyo kwa kuwa miundombinu
itakuwa imeboreshwa vilivyo na itakuwa rafiki wa pande zote
Kwa upande wake mwalimu Rahab Mahenge
alisema uboresha wa miundombinu ya shule hiyo kutachangia kuongezeka kwa ufaulu
kwa kuwa watu wote watakuwa na furaha na mazingira yaliyopo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.