Waziri wa madini Doto Biteko alisema hayo kwenye mkutano wa nane wa Kidunia wa uwazi na uwajibikaji unaofanyika jijini Paris Ufaransa kuwa, Tanzania imetekeleza vyema mkakati wa uwazi na uwajibikaji kwenye kulinda rasilimali za Nchi kwa kuifanyia marekebisho sheria ya madini ya mwaka 2010 ili iendane na matakwa ya mkakati huo.
Katika kuhakikisha uwazi unakuwepo serikali iliamua kufanya marekebisho na pia kuanzisha sheria ya uwazi na uwajibikaji ya mwaka 2015 ili kuweka jambo hilo kisheria.
Pia wakati akijibu swali toka kwa wachangiaji alisema kuwa, hatua ya seikali kuanza kuweka sheria mbali na mikataba kwenye tovuti ni hatua ya mafanikio ambayo inaongesha utayari na katika kuhakikisha watanzania wanajua madhui zaidi ya sheria hizo na mikataba basi ni wazi kuwa uwepo wa asasi za kiraia unaonekana hapo kwa kuwa zinawajibu wa kufanya kazi na serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanafikia na kupata kujua nini kimeandikwa ndani ya mikataba hiyo.
Biteko ameeleza kuwa Tanzania ipo tayari kuemdelea kutekeleza makakti huo na pia hata Nchi nyingine zije kujifunza toka Tanzania.
Mkutano huo wa kidunia unajumuisha zaidi ya washiriki 1000 na nchi 100 zinazokutana na kujadili utekelezaji wa mkakati huo.
Washiriki toka Tanzania wametoka serikalini, asasi za kiraia na waandishi wa habari.
Shirika la kimataifa la Hivos Afrika ya mashiriki lilichukua jukumu la kuwasafirisha baadhi ya washiriki tika asasi za kiraia na waandishi wa habari ili wahudhurie mkutano huo na kuongeza weledi wa kufuatilia uwazi na uwajibikaji kwenye kulinda rasilimali za Nchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.