ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 25, 2024

MWENEZI MRAMBA ASHUSHA NONDO KWA VIONGOZI WA TAASISI ZISIZOKUWA ZA SERIKALI


NA VICTOR MASANGU, PWANI
Katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Pwani David Mramba amewataka viongozi wa taasisi zisizokuwa za kiserikali kuachana na tabia ya kubezana na badala yake wanapaswa kuwa na umoja,mshikamano na kuwa wazalendo na Taifa lao.

Mramba ameyasema hayo wakati wa kikao maalumu ambacho kimewakutanisha   taasisi mbali mbali zisozokuwa za kiserikali kwa ajili ya kujadili mambo pamoja kupewa elimu juu ya mambo mbali mbali mbali ikiwemo mambo ya mikopo,mahusiano, elimu ya uchaguzi wa serikali za mitaa,mizani ya kazi,pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Mramba alisema kwamba taasisi hizo zinapaswa kuweka mipango madhubuti katika kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujenga mahusiano mazuri na taasisi nyingine.

Pia alitaka taasisi hizo zifanye kazi kwa maslahi ya Taifa na sio kufanya kazi kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja lengo ikiwa ni kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

"Kitu kikubwa ambacho kinatakiwa kwa taasisi ni kuwa na umoja pamoja na kuwa wazalendo na nchi yao na kuachana kabisa na mambo ya kubezana kitu ambacho sio kizuri na kuwahumiza kuzidi kushirikiana katika kila jambo,"alisema Mramba.

Aidha Katibu huyo alimpongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu kwa kuweza kutenga fedha nyingi kwa ajili wa utekelezaji wa miradi mbali mbali kwa wananchi wake.

Alibainisha kwamba Rais amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo katika nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya elimu,afya,maji miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyingine za kijamii.

Katika hatua nyingine Katibu huyo ameagiza tasisi  zote ambazo sio za kiserikali katika   Mkoa wa Pwani kuhakikisha kwamba  zinajisajili zote  ifikapo Juni 30 mwaka huu ili ziweze kutambulika na kuweka mipango mikakati ya kufanya kazi.

Katika kikao hicho maalumu  kimehudhuliwa na viongozi mbali mbali kutoka taasisi 22  zisizokuwa za kiserikali sambamba viongozi wa (CCM) kutoka  mikoa ya Ruvuma,Morogoro,Dar es Salaam pamoja na wenyeji Mkoa wa Pwani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.