NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Baada ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dkt Angeline Mabula kutoa malalamiko yake katika Bunge la 12 Mkutano wa 15, kikao cha 12 kuhusu changamoto zilizopo katika shule ya msingi Kitangiri ambayo inakutumika vibaya nyakati za jioni na 'madada powa' wakifanya biashara ya ngono kwenye eneo hilo na kuomba Wizara husika itenge fedha kwaajili ya ujenzi wa uzio kwa shule hiyo ili kuokoa maisha ya watoto wanaochezea 'kondomu' kama mpira. Wakati zoezi la ujenzi wa ukuta kwa shule hiyo likifanyika, hatimaye kipindi cha 'Drive Mix' kutoka radio Jembe Fm kinapata nafasi ya kuzungumza na diwani wa kata hiyo Mhe. Donard Ndalo Protas ambaye naye anatiririka haya akitusanua pia uwepo wa Makaka poa'. "Ilikuwa ni aibu kwasababu hawa madada powa na makaka powa walikuwa wakifanya biahsra yao ya kujiuza maeneo ya shule ndani ya shule, kwenye madarasa, kitu ambacho ni kibaya" "Ni kweli wale walinzi walituhumiwa kuwa na tabia ya kuwapokea hao 'Madada na Makaka poa' kama biashara, wale walinzi walikuwa wakinunua maboksi ya kondom na kuwauzia hao wateja wao, wakifanya biashara mbili, biashara ya kwanza kuwapatia chumba ambacho ni darasa wanalipia na biashara ya pili ni kondom" "Mbaya zaidi mipira hiyo ilikuwa inaachwa ikizagaa maeneo ya shule na watoto wetu walikuwa wakiiokota na kuipuliza, wakifanya mipita ya kuchezea na wengine kama maputo" "Kama kiongozikweli ukipata hii habari ba ukashuhudia mwenyewe kwa macho yako huwezi kuridhika nayo lazima upige kelele"Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.