ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 27, 2024

MEI 28 HADI TAREHE 1 JUNI 2024 NI WIKI YA MAZIWA KITAIFA MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Akizungumza leo hii Tarehe 27 MEI 2024 jijini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewaalika wananchi wa Kanda ya Ziwa, kujitokeza kwa wingi siku ya ufunguzi wa maadhimisho hayo kitaifa katika viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini Mwanza, kwaajili ya kujipatia elimu kuanzia umuhimu wa unywaji maziwa, bidhaa zinazozalishwa na maziwa hadi mbinu bora za ufugaji wenye tija. Bodi ya Maziwa Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na wadau mbalimbali wa maziwa kila mwaka imekuwa ikiadhimisha Wiki ya Maziwa Kitaifa ambayo huwa inafanyika kuanzia mwishoni mwa mwezi Mei hadi mwanzoni mwa mwezi Juni na lengo ni kuwataka wadau mbalimbali nchini kuchangamkia fursa ya kufanya uwekezaji katika sekta ya maziwa kwani uzalishaji ni mdogo ukilinganisha na uhitaji. Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa yakiwa na dhana ya kuhamasisha unywaji wa Maziwa yaliyosindikwa na kuboresha soko la maziwa, dhana hiyo imekuwa ikibadilika na maadhimisho hayo kwa sasa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita yanalenga kuboresha wadau wote walioko kwenye mnyororo wa thamani (Value Chain) kuanzia mfugaji mpaka mlaji. Kuelekea wiki maadhimisho haya malengo makuu ni Kuelimisha wananchi na umma matumizi ya maziwa kama chakula bora kwa watu wa rika zote na faida za maziwa katika kujenga afya ya binadamu. Kuwaelimisha wadau kuongeza ubora wa bidhaa za maziwa zinazotengenezwa nchini ,kuwaelimisha wadau umuhimu wa kujiunga na vyama vya Ushirika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.