ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 1, 2024

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA MBUNGE KOKA KWA KUFIWA NA BABA YAKE MZAZI



NA VICTOR MASANGU,MOSHI KILIMANJARO 


Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa  Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka kufuatia  kifo cha Baba yake Mzazi Mzee Francis Koka kilichotokea Moshi, Kilimanjaro.


Akitoa salamu za rambi rambi  kwa niaba ya Mhe Rais   Mwakilishi  wake Felister Mndeme alisema ameagizwa na Rais kwenda Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuungana na familia ya Mbunge Koka  kwa ajili ya kuweza kutoa pole na kuungana katika mazishi.


"Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameniagiza kuja hapa Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutoa pole kwa Mhe Koka na kwamba yupo pamoja na familia katika kipindi hiki cha maombolezo,"alisema Mdeme kwa niaba ya Rais.


Mdeme alisema kwamba Rais  Dkt. Samia alitamani kujumuika katika Msiba huo lakini ameshindwa kufika kutokana na kuwepo na majukumu mengine. 


Mwakilishi huyo  wa Rais alibainisha kwamba Mhe Rais anatambua Mchango wa Mzee Francis Koka (WW1 Veteran) na kwamba ni vyema kuenzi historia ya kipekee iliyoachwa na Marehemu ambaye ni Baba Mzazi wa Mhe Koka Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini.


Mazishi ya baba yake mzazi   na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka yamefanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Mkolowony  Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,mawaziri wabunge viongozi wa vyama vya siasa,madiwani,taasisi na mashirika  binafsi pamoja na wananchi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.