ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 31, 2024

SERIKALI YAELEZA NAMNA WALIMU WAPYA WATAKAVYOAJIRIWA

 



Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda akizungumza  wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi uliofanyika Jijini Tanga 
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda akizungumza  wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi uliofanyika Jijini Tanga 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Caroline Nombo akiungumza  
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt Said Mohamed akizungumza 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza 
Meza kuu wakifuatilia 


Na Oscar Assenga, TANGA

SERIKALI imetangaza mkakati wa uboreshaji wa elimu nchini huku ikieleza walimu ambao wataajiriwa ni wale wataokuwa wamefanya mitihani yao na kufaulu vizuri tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wizara ilikuwa ikijaza nafasi zilizokuwa zikihitajika bila kupitia mchakato huo .

Mkakati huo wa serikali umetangazwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi

Alisema kwamba wanaoona jambo hilo sio jema kwao lakini wajiulize kwanini madaktari wanapomaliza Shahada ya kwanza wanalazimika kufanya mitihani ndio wanafanya kazi hivyo suala hilo linapelekwa kwa walimu ili kuweza kupata walimu bora.

Waziri Profesa Mkenda alisema kwamba wanaamini kigezo hicho ndio ambacho kitalivusha Taifa na watahakikisha wanachukua walimu waliobora zaidi na watakaofanya mitihani na kufaulu vizuri.

“Kama tunataka tuboresha elimu lazima twende kwa ujasiri tunapojaribu kuajiri walimu tujiulize tunapigania mwanao apata mwalimu bora sasa tutakapo ajiriw lazima wafanye mtihani na watakaofeli hawatapata nafasi”Alisema

Alisema lakini walimu waliopo watalindwa mpaka watakapostaafu na tutaendelea kuwajengea uwezo kwani Rais anatenga fedha nyingi kwenye elimu halafu tujitenge, haiwezekani lazima tathimini tunayoifanya lazima iendelee na hatua nzuri za baraza hatufurahii kufutia mitihani watahaniwa na waliojaribu kuiba mitihani”Alisema .

Aidha alisema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa Sheria mpya ambayo itawabana watu watakaobainika kuiba mitihani watakamatwa kushtakiwa kwa kesi za uhujumu uchumi na kwenye hilo niwashukuru Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kwa kufanya kazi nzuri wanayoifanya.

“Katika jambo hilo tuzidi kuwa makini tusijikuta tukazubaa tukaanguka Necta msilegeze kamba nendeni kuhakikisha mnalisimamia na takwimu ni muhimu zitatueleza vizuri tunakwendaje na katika hilo tunataka kuimarisha takwimu za elimu Tanzania na kazi hii imeanza na timu ipo kazini”Alisema Waziri Profesa Mkenda

Awali akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Caroline Nombo alilipongeza Baraza la Taifa Mitihani (Necta) kwa taarifa yao ya uwasilishaji wa Taarifa ya Tathimini ya ujifunzaji kwa wanafunzi wa kidato cha pili.

Alisema kwamba taarifa iliyowasilishwa inatoa picha halisi kuhusu na ufundishaji na ujifunzaji kwa shule za Sekondari na msingi nchini na mapendekezoo yaliyotolewa yanaonyesha dira ya nini cha kufanya ili kuhakikisha ufundishaji na ujifunzaji na tathimini katika ngazi ya shule unaimarika.

Alisema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana bega kwa bega na wadau wote wa elimu na baraza la mitihani kuhakikisha masuala yote ya ufundishaji na tahimini yanaimarishwa kwa lengo la kukuza umahiri wa wanafunzi katika masomo hayo.

“Vile Wizara kupitia Baraza la mitihani tutaendelea kuhakikisha kuwa tathimini ya ujifunzaji wa wanafunzi wa kidato cha pili awamu ya pili ya mwaka 2025 itafanyika kwa ufanisi mkubwa”Alisema

Naye kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt Said Mohamed alisema suala la kufanya tathimini ni muhimu ili kuboresha kiwango cha elimu na wamekuwa wakifanya tathmini na mitihani na kueleza tahimini hiyo katika maeneo mbalimbali ni kutaka kujua maendeleo ya wanafunzi wamesoma na wanataka kufika wapi.

Alisema wamesema wameanza kufanya tathimini na masomo manne ambayo yameyafanya wakianzia na somo la kwanza ni Hisabati,Sayansi huku akieleza kwamba katika somo hilo katika mtihani wa darasa la saba mwaka huu utakuwa hauna maswali ya kuchagua

Aidha alisema pia alisema hali ya ufauli nchini ukiangalia takwimu upimaji darasa la nne kwa miaka 10 uliopo ufaulu wa jumla umekuwa juu ya asilimia 80 itapanda kidogo na kushuka,miaka 10 hiyo utaona namna ya watahiniwa imekuwa ikiongezeka .

“Mfano mwaka 2015 darasa la nne laki tisa sasa kwenye usajili wanafikia mpaka 1,800,000 na ufaulu wameendelea kubakia 80 asilimia na namba ya watahiniwa imeongezeka mwaka hadi mwaka”Alisema

Katibu huyo alisema kwa upande wa Daraja la saba ulikuwa ni asilimia 67 mwaka 2015 na umeendelea kupanda na kufikia asilimia 80 mwaka 2023 kimahesabu huo ni ufaulu unaoafanana na bado wameendelea kufika asilimia 80 huku akieleza kwa upande wa Sekondari kidato cha pili ufaulu 2015 mpaka 2023 umekuwa ukiongezeka kutoka asilimia 67 2015 mpaka kufikia asilimia 89 mwaka jana.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.