ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 7, 2011

HII KALI!!..!!

Ni kule Maryland nchini Marekani. Jamaa kavunja na kuingia ndani ya nyumba ili "kuchaji" simu yake. Simu hiyo haikuwa na chaji kwa sababu katika mtaa wake hakukuwa na umeme kutokana na barafu nyingi iliyokuwa imeanguka katika eneo hilo. Basi baada ya kuichomeka simu yake kwenye umeme ili ipate chaja, wenye nyumba wakarejea. Huyoo akakurupuka na kuiacha simu. Polisi wakaitwa na walipopiga baadhi ya namba zilizokuwa kwenye simu hiyo, jamaa akakamatwa kwa ulaini tu!!..

Baadaye imegundulika kwamba kumbe jamaa ni mwizi sugu ambaye ameshawaliza watu kibao katika maeneo hayo na polisi walipokwenda kupiga sachi nyumbani kwake waligundua vitu vingi tu vya wizi. Jamaa anashikiliwa umwelani na dhamana yake imeamriwa iwe 1,100,000.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.