Katika tangazo kupitia televisheni ya taifa, makamu wa rais Omar Suleiman amesema Bw Mubarak amekabidhi madaraka kwa jeshi. Hatua hii imekuja baada ya maelfu ya watu kukusanyika mjini Cairo pamoja na miji mingine mikuu katika siku ya 18 ya maandamano ya kudai Bw Mubarak ajiuzulu.
Waandamanaji walipokea taarifa hizo kwa kushangilia, kupeperusha bendera, kukumbatiana na kupiga honi za magari. "Watu wameuangusha utawala," wamekuwa wakiimba.
MUBARAK NA OMAR SULEIMAN.
"Kwa jina na Mungu mwenye neema, mwenye rehema, raia, katika wakati huu mgumu, Misri inapopitia, Rais Hosni Mubarak ameamua kuachia madaraka kutoka ofisi ya rais ya jamhuri na ametoa jukumu la kuendesha nchi kwa baraza kuu la jeshi," amesema.
"Mungu awasaidie wote," amesema Omar Suleiman.
Bw Mubarak tayari ameondoka Cairo na yupo katika mji wa Sharm el-Sheikh, ambapo ana makazi mengine huko, maafisa wamesema.
Mjini Cairo, maelfu ya watu wamekusanyika nje ya Ikulu, katika eneo la wazi la Tahrir na katika kituo cha taifa cha televisheni. Waandamanaji hao walikuwa na hasira kufuatia hotuba ya Bw Mubarak siku ya Alhamisi. Alikuwa akitarajiwa kutangaza kujizulu, lakini hakufanya hivyo na badala yake kupunguza madaraka yake kwa makamu wa rais.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.