Uongozi wa Bodi ya Waendesha pikipiki jijini Mwanza leo umekutana na wadau wake, jeshi la polisi na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mbunge wa Ilemela kwaajili ya kuzungumzia mstakabari mziwa wa hali ya waendesha pikipiki.
Changamoto mbalimbali zimejadiliwa suala kuu likiwa ni Uvunjifu wa Sheria, ambao umepelekea kusababisha madhara makubwa kwa jamii hususani vifo kwa madereva wenyewe au kwa abiria ambao wamekuwa wakiwabeba.
Tatizo sugu la rushwa nalo lilijadiliwa kwenye mkutano huo uliofurika madereva wa pikipiki.
Elimu ya usalama barabarani nayo ilitolewa kuelimisha madereva wa pikipiki ili kuendesha kwa usalama kwa kuzingatia kanuni.
Vuta picha juu ya umati huu, wote hawa ni madreva wa pikipiki, kwa ukata wa ajira unaoliyumbisha taifa letu, Jeh bila wao kuwekeza kwenye biashara hiyo wote hawa wangekuwa wapi?
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.