Robo fainali itaendelea kesho sambamba na nusu fainali na fainali itakuwa jumamosi.Uongozi wa basketball wa mkoa wa Mwanza unatoa wito kwa wana mwanza wote popote walipo hasa waliopo jijini Dar wajitokeze kwa wingi kuipa support timu yao ya mkoa iwe kwa hali na mali ukizingatia inakabiliwa na ukata kwani wadhamini TBL kupitia Castle lite wametoa shilingi laki 9 tu kwa kila timu hivyo gharama zingine ni juu ya mkoa wenyewe.
Hima hima mwenye maji ya kunywa ayaa, chakula ayaa, nauli ayaa na kulala pia. Timu inaishi Topland hotel Magomeni Mapipa na viwanja vya mashindano ni Don Bosco Upanga na Leaders Club.
Ni chini ya coach Robert Mwita, Timu ya mkoa wa Mwanza inaundwa na wachezaji Bundala Charles, Enock Charles, Ahmed Said, Vincent Shinda, Francis Shilinde, Wilson Sajigwa Masanja, Adam Jegame, Juma Kissoky, Mahamed Ally Dibo, Amri Mohamed, Amon Diba Semberya, Chacha Mukolo Tubert na Kizito Sosho Bahati.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.