ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 15, 2011

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA WATANGAZA HABARI NJEMA KWA WATANZANIA

Wakati wa kuadhimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara Ubalozi wetu nchini Uingereza ukishirikiana na Chuo Kikuu cha mji Coventry wanapenda kuwatangazia wadau wote wa elimu kuwepo kwa Scholarship sita maalum za masomo kwa watanzania ambazo zimetolewa kutoka katika Chuo kikuu cha Coventry katika nyanja zifuatazo:

1. MSc Oil & Gas Management
Coventry Campus
Kuanzia Septemba 2012

2. MBA Oil & Gas Management
London Campus
Kuanzia April, July, Septemba 2012

3. MSc Finance & Investment
IAA Dar Campus
Kuanzia Septemba 2012

4. MBA Logistics
IAA Dar Campus
Kuanzia Septemba

5. MSc Finance & Investment
IAA Arusha Campus
Kuanzia Septemba 2012

6. MBA Logistics
IAA Arusha Campus
Kuanzia Septemba 2012

Jinsi ya kujiandikisha, tembelea tovuti ifuatayo:

http://www.coventry.ac.uk/tanzania2012scholarship

ZAIDI ya hayo Ubalozi wetu ukiwakilishwa na Balozi Mh Peter kallaghe, Chabaka Kilumanga na Allen Kuzilwa, ulipata fursa pekee ya kukutana na kumpongeza afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndg. Semu Mwakyanjala ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya Pili( Masters Degree in Communication, culture & Media) katika chuo kikuu cha Coventry alieshinda tuzo ya kuandika insha kuelezea jinsi gani nchi ya Ujerumani itakavyokua mwaka 2051.

Aidha Mh. Balozi Kallaghe alimpongeza sana Afisa Semu kwa juhudi zake kwa kufanikiwa kushinda tuzo hii na kuiletea heshima Tanzania Ughaibuni na kuwahamisisha watanzania wote kusoma na kufanya kazi kwa bidii zaidi. Wakati akiongea na waandishi wa Habari afisa Semu alianza kwa kutoa shukrani kwa familia yake, wafanyakazi wenzake kutoka TCRA na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kumwezesha kufikia hatua aliyopiga leo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na ubalozi wetu hapa London 00 44 20 7569 1470

Tafadhalini watanzania wote chukueni hii nafasi mapema iwezekanavyo kwa wale wote mnaopenda kujiendeleza kimasomo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.