Takriban watu 20 waliuawa katika makabiliano ya siku ya Jumatatu. Licha ya fujo, uchaguzi ulifanyika, lakini idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura inasemekana kuwa ndogo.
Serikali inasema kuwa uchaguzi umekuwa huru zaidi kuliko miaka iliopita, lakini upinzani ulitoa wito wa kususia uchaguzi na kuanzisha mgomo.
Shirika la habari la serikali nchini Syria linasema watu wengi wamejitokeza katika vituo vya kupiga kura, Lakini katika ngome za upinzani wanaharakati wanasema hakuna dalili kama uchaguzi unafanyika, na hata pengine hakuna hata mmoja anayepiga kura, mwandishi wa BBC Jonathan Head aliye nchi jirani ya Uturuki anasema.
Navi Pillay anaelezea hali nchini Syria kama "isiyoweza kuvumiliwa" na kusema kuwa mateso dhidi ya binaadamu huenda yalifanyika.
Bi Pillay anasema makadirio yake ya mauaji ya watu zaidi ya 5,000 hayajumuishi maafisa wa usalama. Serikali ya Syria inasema kuwa zaidi ya maafisa 1,000 wa polisi na jeshi wameuawa.
Chanzo bbc swahili
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.