ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 2, 2018

WAARABU WATIBUA MIPANGO YA CHIRWA KUTUA SIMBA.

Huku taarifa za chini kwa chini zikielezwa kuwa Simba inamuwinda kwa udi na uvumba mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, imeelezwa waarabu wameingilia kati mpango huo.

Klabu ya Ismailia ya Misri imeingilia rada za Simba kuhusiana na usajili wa Mzambia huyo ambapo taarifa zinasema imeanza mazungumzo ya kuweza kumnyaka mchezaji huyo tegemeo kwa Yanga.

Chirwa ameshindwa kujumuika na kikosi cha Yanga kuelekea Kenya kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza kesho.

Waarabu hao wameanza kuifanyia umafia Simba ambapo inaelezwa wameandaa dau nono zaidi ya Simba hivyo kuweka ugumu wa kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi ambao wanatajwa kupigania saini yake hivi sasa.

Mzambia huyo amekuwa akiwindwa na Simba ingawa mwenyewe amekuwa akieleza kuwa anatamani kucheza soka la kimataifa hivyo kuna hatihati kama anaweza akasalia Tanzania msimu ujao.

Uwezekano mkubwa wa Chirwa kuondoka Yanga unawezekana kutokana na mchezaji huyo kugoma mara kadhaa kusafiri na timu pale inapotoka kwenda nje ya nchi kushiriki mashindano ya Kimataifa, ikielezwa kuwa anaidai stahiki zake ikiwemo mishahara.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.