Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akitoa ufafanuzi mbele ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa kujadili nafasi ya Asasi za kiraia katika chaguzi zijazo hapa nchini.
Asasi za
kiraia nchini zimetakiwa kujitoa katika kuhakikisha wananchi wanashiriki kwa
wingi katika chaguzi mbalimbali ikiwemo ya serikali za mitaa na wa serikali kuu
wa mwaka 2020.
Hayo yamesemwa
mapema leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil
Society Bw. Francis Kiwanga alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi, wenye
lengo la kujadili hali ilivyo kabla ya kufikia uchaguzi wa serikali za mitaa
unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani.
Mzee Gallus Abeid kutoka Mwalimu Nyerere Foundation akichangia mjadala mapema leo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Uchaguzi ulioandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Foundation for Civil Society.
Bwana Kiwanga
amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika kupiga kura umekuwa ni mdogo sana
kwani 2010 wamepiga asilimia 43 peke yake na kwa mwaka 2015 ni asilimia 67 ya
wananchi wote wenye sifa za kupiga kura.
Baadhi ya washiriki kutoka asasi mbalimbali za kiraia wakifuatilia kwa umakini mkutano.
Ameeleza kuwa hii inatokana na wananchi kutokuwa na imani na viongozi wanaochaguliwa kwani wanaamini hata usipopiga kura basi mgombea wa chama fulani atapita kwa njia yeyote ile, hivyo taasisi zinazohusika ikiwemo wizara ya tamisemi na NEC pamoja na ZEC kuboresha utendaji wao wa kazi ili kurejesha imani hiyo kwa wananchi.
Amesema kuwa asasi za kiraia zina jukumu kubwa la
kushirika katika mchakato kabla, kipindi chenyewe cha uchaguzi na baada ya
uchaguzi kwa kuwapa hamasa wananchi lakini pia kuomba nafasi za uangalizi
katika kipindi hicho.
Wageni waalikwa wakifuatilia mkutano kwa umakini.
Kwa upande
wake Mzee Gallus Abeid kutoka Mwalimu Nyerere Foundation amesisitiza uwepo wa
amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi kwani amani ndio msingi
wa mambo yote.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa uchaguzi ulioandaliwa na shirika la Foundation for Civil Society wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo jijini Dar es salaam.
Amesema kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa hivyo inapotokea watu wanamchagua mgombea Fulani alafu matokeo yanabadilishwa na kupewa mtu mwingine hii sio sawa na inaweza kutowesha amani ya nchi
Lakini pia
hali ya mtu anatumia muda mwingi kwenye foleni ya kujiandikisha na mwisho wa
siku anaenda kupiga kura anaambiwa jina lako halipo kwenye daftari hali hii
inasababisha watu wengi kuacha kujiandikisha kupiga kura na kupoteza haki yao
ya msingi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.