ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 30, 2018

CHAMA TAWALA DRC CHAMUANDALIA KABILA MAZINGIRA YA KUGOMBEA MUHULA WA TATU.

Chama tawala katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kimemuandalia Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo mazingira ya kugombea urais kwa muhula wa tatu, licha ya lalama na makelele kutoka vyama vya upinzani.
 Ingawaje Rais Kabila amekuwa akikwepa kujibu swali kuhusu iwapo atawania muhula wa tatu au la, lakini chama tawala cha People’s Party for Reconstruction and Democracy (PPRD) kimebandika mabango yenye picha za kiongozi wao huyo kuanzia mijini hadi vijijini,miezi miwili kabla ya uchaguzi wenyewe.
Aidha chama hicho tawala kimetengeneza fulana zenye picha za Kabila na kuzigawa kwa watu katika kila kona ya nchi, na haswa ngome za kisiasa za rais huyo. 
Wapinzani wanasema Kabila ambaye mwezi huu aliwapiga kalamu nyekundu baadhi ya majaji wa Mahakama ya Katiba na kuteua wengine wapya, hapaswi kugombea urais wa muhula wa tatu.
Hii ni katika hali ambayo, utafiti wa shirika la Congo Research Group CRG likishirikiana na Kituo cha Utafiri wa Maoni cha BERCI,  unaonyesha kuwa kwa kila raia kumi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanane hawamungi mkono Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo.
Wananchi wakiandamana dhidi ya Kabila
Utafiti huo unaonesha kuwa, akthari ya Wakongomani wamechoshwa na uongozi wa miaka 17 wa Rais Kabila na wanataka kumuona akiachia ngazi.
Joseph Kabila alikataa kuachia madaraka baada ya kumalizika muhula wake wa utawala kikatiba mwaka 2016, na mpaka sasa hajajitokeza hadharani kusema iwapo atagombea au ataachia ngazi baada ya uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanyika Disemba 23 mwaka huu au la.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.