Wafanyakazi wakijiandaa kuanza zoezi la kupanda miti wilayani Siha, Kilimanjaro.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL waliopo katika mafunzo ya kukuza vipaji wakishiriki zoezi la kupanda mito wilayani Siha, Kilimanjaro.
Wafanyakazi wakipanda miti wilayani Siha, Kilimanjaro.
Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group, George Kavishe akiongea wakati wa tukio la upandaji miti
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba wakati wa hafla hiyo
Na Mwandishi Wetu.
*Kushirikiana na Kilimanjaro Project kupanda miti 100,000 mkoani humo.
Kampuni ya TBL Group imeshiriki zoezi la kupanda miti wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, ukiwa ni mwendelezo wa mkakati wake wa pamoja na taasisi ya Kilimanjaro Project na wadau wengine, kupanda miti 100,000 mkoani Kilimanjaro, katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
Zoezi la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani limeongozwa na Mkuu wa wilaya ya Siha, Mheshimiwa Onesmo Buswelu, ambaye alisema kuwa jukumu la kutunza mazingira ni la kila mmoja na kupongeza kampuni ya TBL Group na wadau wake kwa jitihada wanazofanya kulipa kipaumbele suala la kutunza mazingira.
Alisema katika miaka ya karibuni Tanzania imekuwa ikikabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yametokana na athari za uharibifu mbalimbali wa mazingira kama vile, kukata miti ovyo,shughuli za kilimo kisicho na mpangilio.Moja ya eneo lililoathirika na uharibifu wa mazingira alilitaja kuwa ni maeneo yanayozunguka mlima Kilimanjaro.
Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga, alisema ili kukabiliana na changamoto ya kudhibiti uharifu wa mazingira mkoani Kilimanjaro, kampuni ya TBL kwa kushirikiana na taasisi ya Kilimanjaro Project imejiwekea malengo ya kuunga mkono jitihada za serikali za kudhibiti uharifu kwa mazingira kwa kujiwekea malengo ya kupanda miti 100,000 katika mkoa wa Kilimanjaro katika kipindi cha miaka 10 ambao imeanza kuutekeleza
Tenga alisema, idadi ya mamilioni ya miti inakatwa kila mwaka mkoani Kilimanjaro pia hekari zipatazo 300,000 za ardhi zinakatwa miti kwa ajili ya mkaa na kuni na shughuli nyinginezo za kilimo,takwimu hizi zinatoa tahadhari kuwa hatua za kulinda mazingira zinapaswa kuchukuliwa “Katika kipindi cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka huu tunaanza hatua ya awali ya kupanda miti milioni moja”,alisistiza.
Mwasisi na Kiongozi wa mradi huu, Sarah Scottt, kutoka taasisi ya Kilimanjaro Project amesema “Maandalizi ya kufanikisha mpango huu yanaendelea vizuri,hatua za awali za kuotesha mbegu za miti na kuainisha maeneo ya kupanda miti na mikakati ya kuitunza ili isitawi yanaendelea vizuri. Tunaamini tukiungaisha nguvu kukabiliana na changamoto hii tunaweza na kurejesha hali nzuri ya hewa mkoani Kilimanjaro ilivyokuwa hapo awali na mvua za uhakika kupitia kupanda miti kwa wingi”
Mradi huu kwa upande wa TBL Group utatekelezwa na chapa yake ya Bia maarufu ya Kilimanjaro Lager. Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group, George Kavishe amesema “Kupitia bia ya Kilimanjaro tutaelimisha jamii juu na elimu hiyo itahusu uhamasishaji wa kupanda miti kwa wingi,kutunza mazingira ya asili na kuhamasisha kila mmoja kuwajibika na utunzaji wa dunia yetu tunayoishi”,alisema Kikuli.
Ili kufanikisha lengo ya upandaji miti milioni moja,TBL Group na taasisi ya Kilimanjaro Project zinakaribisha mashirika na kampuni nyingine za biashara ikiwemo na watu binafsi kushiriki katika kampeni hii na kupanda miti Kilimanjaro. TUJE PAMOJA! Tushirikiane kwa kuonyesha vitendo ili kufanikisha kuleta mabadiliko change!
Mbali na kupanda miti mkoani Kilimanjaro, TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBev imekuwa mstari wa mbele kutekeleza sera ya kulinda mazingira kwa kuhakikisha inatumia uzalishaji kwa kutumia mifumi isiyoharibu mazingira sambamba na kushiriki kutoa elimu ya kulinda mazingira na vyanzo vya maji.Vilevile wafanyakazi wake wamekuwa mstari wa mbele kushiriki katika miradi mbalimbali ya utunzaji wa mazingira.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.