Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akihutubia wakati wa kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
(Picha zote na Mathias Canal)
Na Mathias Canal, Zanzibar
Kongamano lilodumu
kwa siku mbili kwa kuwakutanisha watanzania waishio Ughaibuni (4th Tanzania
Diaspora Conference) limehitimishwa hii leo Agosti 24, 2017 huku likiwa
limehudhuriwa na Diaspora 350 na kuchagizwa na wahudhuriaji wengine ambao ni
watendaji kutoka taasisi za serikali na wadau katika uwekezaji na uchumi.
Kongamano la nne
la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) lilifunguliwa
jana tarehe 4 Agosti 2017 na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri
ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan ambapo limefikia ukomo kwa
kupatikana majibu ya changamoto mbalimbali ziwahusuzo Diaspora ikiwemo uraia
pacha na sera ya utambuzi wao nchini Tanzania.
Akihutubia mamia
ya watanzania walioshiriki katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama
Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome
kongwe-Zanzibara, Makamu wa pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd alisema kuwa serikali
inawatambua Diaspora kama mabalozi muhimu katika kutangaza utalii Duniani kote
jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaongeza kipato cha nchi.
Alisema kuwa serikali inatambua
kazi kubwa inayofanywa na Diaspora katika kuitangaza nchi ya Tanzania na
vivutio vyake hivyo kuwataka kutumia fursa hiyo pia kuwatangaza viongozi wa
serikali kwa weledi mpana pasipo kueneza chuki dhidi ya viongozi wao.
Mhe alozi Seif alisema kuwa kumekuwa na
watanzania waishio nje ya nchi wasiokuwa na weledi na nidhamu dhidi ya viongozi
wa serikali kwani wamekuwa wakiwasema vibaya kwa kuwatukana na kejeli jambo
ambalo linarudisha nyuma heshima yao waliyonayo na kutia doa serikali.
Alisema kuwa
Diaspora wanapaswa kuendelea kushiriki katika makongamano mengine yajayo kwani
kufanya hivyoi kunatoa fursa kwao kuishauri serikali na kuona namna bora ya
utambuzi wao.
Alisema serikali
itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya
uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji
katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio
nchini na Taifa kwa ujumla wake.
Alisema kuwa ushirikiano
huo wa Diaspora kupitia makongamano yote yaliyopita umeimarisha zaidi mahusiano
chanya bila kujali dini wala kabila jambo ambalo limeongeza utu, umoja na
mshikamano.
Mhe alozi Seif
alisema kuwa Diaspora wanatakiwa kuheshimu sheria, taratibu na taratibu za nchi
wanazoishi ili kue delea kuipatia sifa chanya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Naomba nikukumbusheni nyote
mliohudhuria hapa hii leo kutamnbua kuwa mchumia juani hulia kivulini nanyi
kivulini kwenu ni hapa nyumbani hivyo tumie fursa ya uwekezaji vizuri huku
mkikumbuka kuwa mkataa kwao ni mtumwa zaidi endelezeni umoja na mshikamano
kwani inafahamika kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.” Alisema Balozi
Seif Ally Idd
Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) linaratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusudio la kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) linaratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusudio la kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano kama hilo linaakisi
makongamano matatu ya utangulizi yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es
Salam huku kongamano la mwaka 2016 na mwaka huu 2017 yakifanyika visiwani
Zanzibar huku likiwa limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo”
chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”
Kongamano la
watanzania waishio ughaibuni kwa mwaka 2017 limedhaminiwa na PBZ Bank, ZSSF,
Idara ya Uhamiaji, Sea Cliff Hotel, CRDB Bank, Mult Colour, Equity Bank,
Zanzibar Cable Television, ZBS, Watumishi Housing Cooparation na Petro.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Issa Haji Gavu akitoa salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga Kongamano la nne
la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama
Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome
kongwe-Zanzibara.
Washiriki wa Kongamano la nne
la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia hotuba ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama
Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome
kongwe-Zanzibara.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy (Kushoto) akifatilia burudani mbalimbali wakati wa kufunga Kongamano la nne
la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla
ya chakula cha jioni iliyojulikana kama
Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome
kongwe-Zanzibara, Mwingine ni Balozi Anisa Mbega Mkurugenzi wa Idara ya
Diaspora Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akihutubia wakati wa kufunga Kongamano la nne
la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama
Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome
kongwe-Zanzibara.
TAZAMA PICHA ZAIDI
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.