ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 26, 2017

MARUFUKU YA MIFUKO YA PLASTIKI KUTEKELEZWA KENYA KUANZIA AGOSTI 28.


Serikali ya Kenya imetanagaza kwamba marufuku ya mifuko ya plastiki itaanza kutekelezwa Jumatatu Agosti 28 kama ilivyopangwa.
Katibu katika wizara ya mazingira, Charles Sunkuli amesema makataa ya marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki hayatabadilishwa licha ya malalamiko ya watengenezaji bidhaa hiyo. Katibu huyo alisema marufuku hiyo inafanyika kwa mujibu wa katiba ambayo inampa kila Mkenya haki ya kuishi katika mazingira safi.
Sunkuli alisema tayari serikali imechukua hatua za kupunguza utengenezaji au uagizaji wa mifuko ya plastiki na inashirikiana na serikali za kaunti kubuni sera kuhusu kupunguzwa kwa matumizi ya mifuko hiyo. Aidha amesema serikali za kaunti kuhakikisha zimebuni sheria za kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki. 

Alisema Wakenya hawana budi ila kutafuta njia mbadala za kubeba bidhaa kwa lengo la kuhifadhi mazingira. 

Watengenezaji bidhaa wamedai kwamba marufuku dhidi ya mifuko ya plastiki itaathiri moja kwa moja takriban nafasi elfu 60 za ajira na nyingine laki 4 zisizokuwa za moja kwa moja. Hata hivyo serikali imekanusha ikisema mikakati kabambe imewekwa ili kuwalinda.

Harakati ya kuunga mkono marufuku ya mifuko ya Plastiki Kenya.
Kulingana na waziri wa mazingira nchini Kenya, Prof Judy Wakhungu mazungumzo kuhusiana na karatasi hizo yalianza miaka 15 iliyopita licha ya kwamba shirikisho la muungano wa watengenezaji wa bidhaa Kenya linaomba kupewa muda zaidi kutafuta njia mbadala.
Kwa mujibu wa sheria mpya, atakayekiuka marufuku ya mifuko ya plastiki hiyo anawezwa kutozwa faini ya kati ya shilingi milioni mbili na milioni nne pesa za Kenya (Dola 20,000-40,000 za Marekani) ama kifungo cha kati ya mwaka mmoja na miaka minne gerezani, au adhabu zote mbili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.