NA ALBERT G. SENGO:MWANZA
Ikicheza nyumbani Timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza leo imefungwa mabao 2-1 na Kagera Sugar toka Bukoba mkoani Kagera katika mchezo wa kiporo ligi kuu soka Tanzania bara ulioahirishwa kuchezwa siku ya jumatano kufuatia mvua kubwa kunyesha na hali ya uwanja wa CCM Kirumba kuwa tete.
Toto ilionyesha uhai kwenye dakika za mwanzo za mchezo na kufanikiwa kupata bao dakika mbili tu tangu kipyenga cha kuanza mchezo kilipo pulizwa mfungaji akiwa ni Peter Mtabuzi.
Dakika ya kumi ya kipindi hicho cha kwanza tayari Kagera Sugar walikuwa wamelifikia lango la Toto na kusawazisha kupitia Temu Felix.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Toto 1, Kagera Sugar 1, goli la ushindi kwa Kagera Sugar lilipatikana mnamo dakika ya 56 mfungaji akiwa ni Daudi Jumanne.
Kocha wa Kagera Sugar Abdalah king Kibadeni amezungumza na Sports Xtra na haya ndiyo aliyosema bofya play hapo chini....
|
Abdalah Kibadeni |
|
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.