JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu
“MKUUPOLISI”
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734
Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na.(022)2135556
S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:
DAR ES SALAAM.
02 Septemba 2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MABADILIKO KWA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI.
Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini IJP Said Mwema, amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa
Polisi wa mikoa na vikosi.
Mabadiliko hayo ni
pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani SACP Ernest Mangu
anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kuziba pengo la marehemu ACP
Liberatus Barlow, ACP David Misime aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke
kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya SACP Zelothe
Steven anayestaafu. Vilevile, aliyekuwa kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege ACP
Ulrich Matei anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani.
Aidha, wengine ni
kutoka Makao Makuu ya Polisi na Makao Makuu Idara ya Upelelezi ambapo ACP
Engelbert Kiondo kutoka makao makuu Idara ya Upelelezi anakwenda kuwa
kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, ACP Rashid Seif kutoka Makao Makuu ya Polisi
Kwenda kuwa Kamanda wa kikosi cha Tazara, ACP Deusdedit Kato kutoka Makao Makuu
ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, ACP Shaban Hiki
kutoka Kamanda wa Kikosi cha Ufundi kwenda Makao Makuu ya Polisi na ACP Lucas
Mkondya kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Kikosi cha Ufundi.
Mabadiliko hayo
pia yamehusisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa kikosi cha Usalama
Barabarani ACP Johansen Kahatano anayekwenda kusimamia Mradi wa
SMARTER Traffic ambapo nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa RTO mkoa wa Pwani
ACP Swalehe Mbaga. Uhamisho huo pia umewahusisha baadhi ya Wakuu wa Operesheni
wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi vya Kutuliza Ghasia vya Mikoa, Wakuu wa Polisi wa
Wilaya na Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya.
Uhamisho huo ni wa
kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-ASP
Msemaji wa
Jeshi la Polisi (T).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.