ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 31, 2012

WATUHUMIWA KESI YA MAUAJI KAMANDA WA POLISI MWANZA WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

Zoezi la utambuzi wa wahusika wa mauaji.
Watuhumiwa watano wa mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow leo majira ya mchana saa 8:55 wamefikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali kusomewa mashitaka yanayowakabili.

Watu hao ni Muganyizi Michael Peter (36), Chacha Waitare Mwita (50), magige Mwita Marwa (48), Bugazi Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42).

Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu mfawidhi wa serikali Kastus Ndamugobi amesema kuwa watuhumiwa hao wanakesi ya jinai la Mashitaka ya mauaji namba 30 kifungu cha 196 na 197 cha kanuni ya adhabu ya sheria iliyofanyiwa marekebisho ya mwaka 2002, kwani mnamo October 13 usiku walishirikiana kumuua mtu mmoja aitwaye Liberatus Barlow katika eneo la Minazi Mitatu Kitangili wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Mwendesha mashitaka huyo akitaja kuwa upelelezi bado ungali ukiendelea ameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo.

Ombi hilo limekubaliwa na sasa kesi hiyo imepangwa kusomwa tena tarehe 15 November 2012.  

Watuhumiwa hao waliondoka eneo hilo la mahakama chini ya ulinzi mkali huku wakiwa wamemshikilia huku na huku mtuhumiwa mwenzao Muganyizi Michael Peter (aliyetajwa na wenzie kuwa ndiye aliye mpiga risasi na kumuua Kamanda Barlow) anayetembea kwa taabu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.