Mtoto Asfati Mslam amefariki dunia leo majira ya saa 9 na dakika kadhaa alasili katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure alikokimbizwa yeye na wazazi wake mara baada ya kuumizwa vibaya kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kupitia mawe yaliyoporomoka kutoka kwenye msingi wa nyumba iliyo eneo la juu mlimani jijini Mwanza.
Kuangukiwa nyumba hiyo ni tukio lililotokea leo hii majira ya asubuhi saa 5:45 katika nyumba wanayoishi kilima cha Sabato mtaa wa Ngara eneo la Mlimani 'B' Kirumba jijini Mwanza ambapo pamoja na kwamba ni majira ya mchana watu hao mke na mume walikuwa wamejipumzisha chumbani wakiwa na mtoto wao, (yawezekana kutokana na hali ya hewa kwa mvua inayoendelea kunyesha leo tangu asubuhi hadi muda huu tunakupa taarifa) ndipo wakakutana na ajali hiyo.
Msingi wa nyumba iliyo eneo la kimo cha juu toka nyumba iliyovunjwa ukuta na kutokea ajali.
Wananchi wakiwa wameizingira nyumba liyovunjwa ukuta na kusababisha dhahma hiyo iliyo ondoa uhai wa mtoto Asfati Mslam huku wazazi wake wakiwa katika hali taabani hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza.
Hii ndiyo nyumba ambayo kuta zake zilibomolewa na mawe ya msingi wa nyumba iliyo juu yake.
Mashuhuda wakiwa wameambatana na mwenyekiti wa mtaa wa Ngara Kirumba eneo la mlimani 'B' Bw. Thadeo Katalala.
Kaburi la Asfati. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.