Mojawapo ya vimbunga
vikubwa zaidi kuwahi kupiga Mashariki mwa Pwani ya Marekani kimesababisha
mafuriko makubwa katika baadhi ya sehemu za mji wa New York.
Maeneo mengi mjini
yamewachwa katika giza baada ya huduma za umeme kukatizwa.
Kimbunga hicho
kilipiga ardhi kwenye Pwani ya New Jersey karibu na mji wa Atalanta muda mfupi
jana usiku/Dhoruba kali kutoka mjini Florida hadi nchini Canada imepiga
Mashariki mwa Marekani na kusababisha mawimbi makali mjini New York.
Maji yamefurika kwenye
barabara na katika njia za reli pamoja, maeneo ya kuegesha magari na katika
eneo la Ground Zero, eneo ambalo mashambulizi ya Septemba kumi na moja yalitokea.
Sehemu kubwa za mji wa
New York ziko kwenye giza baada ya milingoti ya umeme kuharibiwa.
Wagonjwa waliondolewa
kwenye hospitali moja baada ya umeme kukatika.
Zaidi ya watu milioni
tano walisemekana kukosa umeme katika eneo la Pwani baada dhoruba kali huku
takriban wengine milioni moja wakishauriwa kuhama nyumba zao. Athari za
kimbunga hicho labda huenda zikajulikana baadaye leo.
CHANZO: bbc swa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.