Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akifafanua uchafuzi unaofanywa na baadhi ya wanunuzi na wakulima kwa kuchang’anya pamba, maji, mchanga na mbegu kwa lengo la kuongeza uzito. |
Mbegu zilizochanganywa kenye pamba kwa lengo la kuongeza uzito |
Ukaguzi ukiendelea kwenye ghala la Pamba. |
Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akionyesha mchanga uliochanganywa na Pamba za moja wa wakulima waliokiuzia kiwanda chake.
|
Ukiitizama kwa harakaharaka pamba hii unaweza kuiona kuwa iko salama, ila ukichukuwa jukumu la kuigusa ndipo utagunduwa kuwa kunachembe chembe za mchanga na uchafu mwingine ndani yake. |
Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akielezea uchafuzi huo ndani ya Pamba. |
Kwa ukaribu zaidi mchanga uliopatikana kwenye Pamba baada ya uchambuzi wa awali. |
Na Peter Fabian
MWANZA.
TATIZO la kushuka thamani ya Pamba nyeupe ya Tanzania (Dhahabu
Nyeupe) kwenye Soko la Dunia na kupelekea kuporomoka kwa bei maradufu
kumeishitua seikali na sasa kupitia Bodi ya Pamba nchini (TCB)imeamua kuchukua
hatua za kunusuru zao hilo kwa kutangaza kuwa kuanzia msimu ujao wa kilimo utakuwa
wa Kilimo cha Mkataba katika Mikoa ya Kanda ya Magharibi.
Hatua hiyo inafuatia tamko la serikali lililotolewa
kwa nyakati tofauti na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa Mkutano wa wadau wa
kilimo cha pamba kutoka Mikoa kumi hapa nchini kilichofanyika mwezi Mei mwaka
huu Jijini humo na lile la Rais Dkt. Jakaya Kikwete alilolitoa wakati wa
majumuisho ya kuhitimisha ziara yake ya siku tano Mkoani Mwanza hivi karibuni.
Mwenyekiti Festus Limbu (katikati). |
“Tumezamilia kurejesha ubora wa Pamba Nyeupe zamani
ikijulikana ‘Dhahabu Nyeupe’ kwa kuhakikisha msimu huu wa Kilimo wa mwaka
2013/2014 unaoanza mwezi Novemba mwaka huu kila Mwekezaji na mnunuzi wa pamba
kuanza kuwekeza kwenye Kilimo cha Mkataba ambacho kimsingi ndiyo kitakuwa
suruhisho la Mkulima kunufaika na Mwekezaji huyo hali itakayosaidia pamba
kurejea kuwa na thamani na ubora” alisema Dr.Limbu.
Mwanyekiti huyo
alisema kuwa utekelezaji wa Mkataba huo utakuwa ni kati ya Wanunuzi,
Wamiliki wa viwanda vya pamba na wakulima ambapo watatakiwa kupeleka kwenye maeneo
ya wakulima vijijini Pembejeo za kilimo ikiwa ni Mbegu za Quton, Mbolea na
Madawa ya kuulia wadudu na kufunga Mkataba na wakulima huku viongozi wa
serikali za vijiji na vyama vya msingi wakiwa mashahidi.
Dr Limbu
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Magu Mkoani Mwanza, alisema tamko la serikali juu ya uamuzi wake wa utekelezaji
wa kilimo cha Mkataba katika tasnia ya Pamba pamoja na kuwa na tija ndogo katika
uzarishaji ambapo uzarishaji kwa umekuwa wa Hekali moja kutoa kilo 300
ikilinganishwa na lengo la kuzalisha kilo 1,500 kwa Hekali moja ifikapo mwaka
2015 kote nchini.
“Tunazo
changamoto nyingi ikiwemo ya uhaba wa viwanda vya kuongeza thamani, matumizi
madogo ya pembejeo, kutolewa kwa pembejeo muda ukiwa umepita, kilimo kutegemea
mvua za msimu na wanasiasa kutumia mwanya wa kujipenyeza na kuwachezea wakulima
jambo ambalo limeonekana kabisa kusababisha ubora hafifu unaosababisha pamba kuuzwe
kwa bei punguzo na kumnyonya mkulima” alisema na kuongeza kuwa
Tasnia ya Pamba ni muhimu katika uchangiaji wa pato la taifa na tegemeo la asilimia 40
ya Watanzania, lakini kilimo cha zao hilo kimekuwa kikikabiliwa na matatizo mengi
na changamoto mbalimbali hali inayoonekana kudidimia kwa zao hilo kila msimu
hivyo kupitishwa kwa mswada wa sheria ya kuanzishwa kilimo cha umwagiliaji
kutakuwa mkombozi kwa wakulima.
“Sekta hiyo
binafsi itabidi iwekeze katika kuwapatia wakulima pembejeo na huduma zingine,
badala ya kusubiri kwenda kununua pamba kwa wakulima mwishoni mwa msimu, kwa
sababu mfumo wa sasa wa mnunuzi kupewa jukumu la kukusanya fedha kutoka kwa
mkulima na kuziwasilisha CDTF umeonekana kuwa na matatizo makubwa” alisema Dr.
Limbu
Aliitaja Mikoa ya Kanda hiyo
itakayo tekeleza kilimo cha mkataba kuwa ni Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Mara,
Kagera, Tabora, Geita, Singida, Rukwa na Kigoma na kwamba wadau wote walio na
nia ya kununua pamba msimu ujao, waanze kusambaza mapema mbegu na pembejeo
(Quton) kwa wakulima ili mwakani wanunue pamba kutoka kwao na si kuvamia
kununua kiholela kama ilivyo sasa.
Mwenyekiti huyo
alisema kuwa Kampuni ya ununuzi wa pamba na kiwanda kitakachoshindwa kupeleka
pembejeo za kilimo kwa wakulima katika utekelezaji wa Kilimo cha Mkataba
kuanzaia mwaka huu wa msimu wa kilimo mwezi Novemba, mwakani waklati wa kuanza
msimu wa ununuzi wa pamba haitapatiwa Leseni na Bodi ya Pamba na halitaruhusiwa
kuvamia kiholela kununua Mikoa yote.
“Leseni za
ununuzi wa pamba zitatolewa kwa kuzingatia kigezo cha uwekezaji wa kila mdau
katika eneo husika na si vinginevyo na hakutakuwa na ujanja ujanja kwenye
kufunga mkataba na wakulima wa zao hilo ieleweke na hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi ya Kampuni husika na wakulima hawataruhusiwa kuuza pamba
yao kwa mtu ambaye hakuwapa pembejeo.
Aidha Dr Limbu alisema kuwa katika kuhakikisha utekelezaji huo unafanikiwa Ofisi za wakuu wa Mikoa,
Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zitasimamia kwa karibu utaratibu huo mpya
wa kilimo cha mkataba ili malengo ya kuondokana na matatizo yanayoathiri kilimo
hicho yafikwe huku wachafuzi wa pamba wakati wa msimu wa kuuza pamba wakiwekewa
mwarobaini wa kuwadhibiti.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.