MWANZA. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amezitaka Televisheni na Redio kuanzia kesho kusoma vichwa vya habari vya magazeti tu ili kuwavutia wasomaji kununua magazeti kwa habari kamili.
Dk Mwakyembe amesema hayo leo jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambapo pia amesema ataendelea kutetea na kulinda haki za waandishi wa habari huku akiwahakikishia ulinzi waandishi wa habari za uchunguzi.
Pamoja na mambo mengine Dk Mwakyembe amehakikisha kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kwa wamiliki wa vyombo vya habari na kwamba ameagiza idara ya mawasiliano kutengeneza mawasiliano ya kudumu na wawe wanakutana angalau mara moja kwa mwezi kujadili udhaifu unaoweza kujitokeza na kuchukua hatua lengo ni kuwekana sawa.
Kuhusu kuzorota kwa hali ya uchumi kupitia mauzo ya magazeti amesema kuwa mchawi wa anguko hilo ni vyombo vya habari hususani radio na magazeti ambapo amevionya vyombo hivyo kuacha kusoma taarifa kwa undani kiasi cha kupoteza umuhimu wa mwananchi kununua magazeti. BOFYA PLAY KUSIKILIZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.