Makumi ya raia wameuawa katika Jamhuri ya
Afrika Kati kufuatia kuzuka mapigano yanayoendelea kushuhudiwa nchini
humo kati ya makundi ya wabeba silaha.
Hayo yamo katika ripoti ya Shirika
la Haki za Binadamu la Human Rights Watch ambayo imefichua kuwa, raia
wapatao 45 wameawa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kutokana na
machafuko yanayoendelea kuikumba nchi hiyo.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa, mapigano
hayo yameyakumba zaidi maeneo ya miji ya Bambari, Ouaka, mkoa wa
katikati na Makoum, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Inaelezwa kuwa, mbali na mapigano hayo kusababisha mauaji makubwa yamepelekea pia wakazi wengi wa maeneo hayo kuwa wakimbizi.
Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mgogoro, mwaka 2013
baada ya kuzuka mapigano ya kikaumu yaliyopelekea kuondolewa madarakani
serikali ya rais François Bozizé.
Hivi karibuni Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa lilitaka kukomeshwa haraka iwezekanavyo, mapigano na vitendo
vya utumiaji mabavu vya makundi ya wabeba silaha, Jamhuri ya Afrika ya
Kati.
Taarifa iliyotolewa na baraza hilo la
usalama la Umoja wa Mataifa mbali na kuonyesha wasiwasi wake juu ya
mapigano hayo nchini CAR, liliyataka makundi ya wabeba silaha hususan
'Harakati ya Kitaifa kwa Ajili ya kufufua nchi FPRC' na kundi la 'Umoja
kwa ajili ya Amani ya Afrika ya Kati UPC' kukomesha uhasama na mapigano
yao nchini humo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.