Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelitaka
kundi la kigaidi la Boko Haram la nchini Nigeria kuhitimisha ukiukaji
wake wa haki za watoto.
António Guterres amesema hayo
katika ripoti yake kuhusiana na hatima ya watoto katika machafuko
yanayoendelea kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na mashambulio ya
kundi la kigaidi la Boko Haram.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema
katika ripoti yake hiyo kwamba, kuna watoto wengi ambao wamekuwa
wahanga wa ngono ambao wamechukuliwa mateka na Boko Haram na
kutumikishwa kama watumwa wa ngono na kundi hilo.
António Guterres ameeleza kuwa, hali wanayokabiliwa nayo watoto katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la kigaidi la Boko Harama inasikitisha mno na kwamba, kuna haja ya kuchuliwa hatua zinazokazolifanya kundi hilo la kigaidi lihitimishe ukiukaji wake wa haki za watoto.
Inaelezwa kuwa, kwa uchache watoto 3900
wameuawa katika hujuma na mashambulio ya kundi la kigaidi la Boko Haram
kuanzia Januari mwaka 2013 hadi 2016 huko nchini Nigeria na kwamba, kuna
watoto wengine 7200 ambao wameuawa kinyama na wanamgambo hao.
Kundi la Boko Haram lilianzisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya umma
na taasisi za serikali huko kaskazkini mwa Nigeria mwaka 2009 na baadaye
mwaka 2015 likapanua mashambulizi hayo hadi katika nchi za Chad,
Cameroon na Niger.Zaidi ya watu elfu 20 wameuwa hadi sasa katika mashambulizi hayo na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.