MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amemshambulia Bashite huku
akisema kuwa mtu huyo alipaswa awe mahakamani na sio ofisini kwa madai
kuwa amefoji vyeti vya elimu ya sekondari jambo ambalo ni kosa kisheria.
Hayo ameyasema leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akichangia hoja kuhusu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Aidha Sugu amemtaka Rapa ROMA Mkatoliki ajitokeze hadharani aeleze wazi
kuhusu alivyotekwa na nani alihusika ili jamii ielewe na mamlaka husika
iweze kuchukua hatua ikiwemo kuwabaini waliyotekeleza tukio hilo ambalo
si la kibinadamu.
Sugu aliwageukia wasanii wa Filamu Bongo ambao hivi karibuni waliandama
wakipinga uingizwaji holela wa filamu za nje ambazo wanadai
zinaporomosha soko la filamu za ndani. Sugu amewataka wasanii hao waache
kutumika kisiasa na badala yake wafate misingi ya kazi zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.