Sumbawanga. Watu watano wamekufa maji katika Ziwa Rukwa lililopo mkoani Rukwa wakati wakiwa katika shughuli za uvuvi ziwani humo.
Tukio hilo lilitokea juzi wakati watu hao wakiwa katika shughuli zao za uvuvi katika ziwa hilo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Polycarp Urio akizungumza leo amesema kuwa watu hao walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika ziwa hilo.
Urio amesema kuwa wavuvi walio kufa maji ni wakazi wa Kijiji cha Ilanga, Kata ya Muze, tarafa ya Mtowisa, wilaya ya Sumbawanga mkoani humo.
Aliwataja wavuvi hao kuwa ni Paschal Kipeza(30), Peter William(45), Edward Emily(40), Frank Kadima(36) pamoja na Saliboko Damasi(28) wote hao wanasadikika kufa maji baada ya boti walilokuwa wakifanyia uvuvi kuzama.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.