NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza
USHAHIDI wa
shahidi wa 16 Vedastus Pius, kesi ya mauji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow umeibua shauri dogo katika kesi kubwa
mahakamani hapo.
Kesi hiyo
imeibuliwa jana katika Mahakama kuu kanda ya Mwanza mbele ya jaji
Sirilius Matupa na wakili wa kujitegemea Maduhu Ngasa baada ya kuonekan
kweny baadhi ya nyaraka za ushahidi kufutika kwa tarehe husika jambo
ambalo lilizua utata na kusababisha kuwepo kwa kesi ndogo.
Baada ya wakili
huyo kutoa hoja zake mtuhumiwa namba sita Abdalla Petro Amos Abdalla
Ndayi (22) alisimama kizimbani kwa ajili ya kutoa ushahidi wake.
Abdalla ameiambia
Mahakama kuwa amefikishwa mahakamani kwa kosa la mauji kesi namba
192/2014 ambapo alikamatwa mnamo Novemba 2 mwaka 2012 saa 12 alfajiri
na kwamba anahusika na mauji ya askari.
"Wakati nakamatwa
sikuelezwa kosa langu na kupelekwa kituo kidogo cha polisi cha Pamba na
nilipofika Pamba niliambiwa kuwa nimekuja kupanga biashara sehemu
ambayo hairuhusiwi nikawekwa ndani siku mbili" amesema Abdalla.
Amesema mnamo
Novemba 4 mwaka 2012 akatolewa na kupelekwa kituo kikubwa cha Nyamagana
na kuwekwa ndani na baada ya hapo walifika askari watatu ambao
hakuwafahamu na kumuita na kwamba hakuitika.
Amesema hakuitika
kwa sababu hayakuwa majina yake na kwamba anaitwa Abdalla Petro ndipo
alitolewa kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo.
" Kutokana na
shahidi wa 16 hauwahi kuniohoji maelezo aliyokuwa akiyaandika ni ya
kwake na baada ya hapo nilisaini kwa shinikizo ili nisiuwawe mnamo
Novemba 5 mwaka 2012 na sio Novemba 3 mwaka 2012 kama shahidi
alivyoeleza" amesema Abdalla.
Aidha baada ya
mtuhumiwa kumaliza ushahidi wake Jaji matupa aliwaruhusu mawakili wa
pande zote mbili kutoa hoja zao kuhusiana na shauri hilo na Jaji
aliihairisha kesi hiyo ambapo uamuzi utatolewa asubuhi hii kabla ya
kuendelea na kesi kubwa ya mauji.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.