Ili
kupunguza vifo vinavyosababishwa na akina mama kujifungulia majumbani kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa Amour
Hemed Hemed amewataka watu wote wenye utamaduni huo kuachana nao ili kunusuru
vifo vitokanavyo na uzazi.
Kiongozi
huyo ametoa rai huyo Wilayani Ludewa kwa wakazi wa kijiji cha Madope mara baada
ya kuzindua jengo la hospitali ya mama na mtoto lililogharimu zaidi ya shilingi
Milioni 37 na kuwataka wanawake wa kijiji hicho wenye utamaduni huo
kuelimishana juu ya madhara ya kitendo hicho.
Nao Wakazi
wa kijiji cha Madope Wilayani Ludewa Mkoani Njombe ambao wamefanikiwa kujenga
zahanati kwa ajili ya kurahisisha huduma za afya kwa kina mama na watoto
wamesema wamekuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita 20 kupata huduma za
afya hali ambayo iliwawia vigumu wajawazito.
Mwenge wa
Uhuru umemaliza mbio zake Mkoani Njombe na kukabidhiwa Mkoani Ruvuma ambapo
ukiwa mkoani Njombe umekagua, umezindua na kutembelea miradi 55 yenye thamani
ya zaidi ya shilingi ya BILIONI 8 na milioni 674.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.